Posts

WATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUZINGATIA VIAPO

Image
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akizungumza leo tarehe 29 Septemba 2026 mkoani Tabora wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na Kata 11 za Tanzania bara.  Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akizungumza leo tarehe 29 Septemba 2026 mkoani Tabora wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na Kata 11 za Tanzania bara.  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima akizungumza jambo wakati wa mafunzo hayo.  Sehemu ya wajumbe wa Management ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wakifuatilia hotuba ya ufunguzi. Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Chamwino Mkoani Dodoma na Kata 11za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ************** Na. Mwandishi Wetu, Ta...

TUME YATANGAZA RATIBA YA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE CHAMWINO NA UDIWANI KATA 11

Image
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza Novemba 04, 2026 kuwa siku ya uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Chamwino, Mkoa wa Dodoma, pamoja na Madiwani katika kata 11 za Tanzania Bara.   Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ramadhani Kailima, imesema uchaguzi huo unafanyika kufuatia kuwepo kwa nafasi wazi za uongozi katika maeneo ya uchaguzi.   “Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu kuwepo kwa nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Chamwino, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma,” ilisema taarifa hiyo.   Nafasi hiyo imetokea baada ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Deogratius John Ndejembi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.   Uteuzi wake ulifanyika tarehe 26 Agosti, 2026 na kuthibitishwa na Bunge tarehe 28 Agosti, 2026. ...

SAPP kufungua Fursa kwa Tanzania Kuwa Kitovu cha Biashara ya Umeme Kusini mwa Afrika

Image
πŸ“ŒNchi 18 Zakutana Zanzibar kujadili usalama wa nishati ya umeme kusini mwa Afrika πŸ“ŒKuuza au kununua umeme kutaongeza mapato ya taifa na kuimarisha usalama wa nishati nchini Na Mwandishi Wetu, Zanzibar Mikutano ya 67 ya Jumuiya ya Umeme ya Kusini mwa Afrika (SAPP) inayofanyika Zanzibar imefungua fursa mpya kwa Tanzania kuimarisha nafasi yake kama kitovu cha biashara ya umeme katika ukanda wa Kusini mwa Afrika, huku ikitarajiwa kuongeza mapato ya taifa kupitia mauzo ya umeme na kuimarisha usalama wa nishati katika ukanda huo. Mikutano hiyo imewakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 18 wa SAPP kwa lengo la kujadili masuala ya biashara ya umeme, uendeshaji wa mifumo ya umeme, uwekezaji katika miundombinu ya nishati na usalama wa nishati katika nchi zilizoko ukanda wa Kusini mwa Afrika. Akifungua mikutano hiyo Septemba 8, 2026 katika Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar, Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), Bw. Haji Mohamed Haji, amesema kuimarishwa kwa uunganishaji wa gridi za ...

TANESCO YABORESHA MAISHA YA WAFANYAKAZI NYUMBA YA MUNGU.

Image
  *πŸ“Œ Nyumba za wafanyakazi zakarabatiwa, kuboresha utendaji wa kazi* *πŸ“Œ Mtambo wa kisasa wa kuchakata maji wazinduliwa* πŸ“ MWANGA, KILIMANJARO | Septemba 2, 2026 Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limezindua na kukabidhi nyumba zilizokarabatiwa kwa wafanyakazi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme kwa Maji cha Nyumba ya Mungu, Wilaya ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro. Nyumba hizo, zilizojengwa tangu mwaka 1969, wakati Kituo cha Nyumba ya Mungu kilipoanza kufanya kazi, zimefanyiwa ukarabati mkubwa hatua inayolenga kuboresha mazingira ya makazi na ustawi wa wafanyakazi. Akizungumza wakati wa uzinduzi na makabidhiano hayo, Afisa Rasilimali Watu wa Kituo cha Nyumba ya Mungu, Bi. Neema Mwaisaka, amewataka wafanyakazi waliokabidhiwa nyumba hizo kuzitunza ili ziendelee kuwa na thamani na kutumika kwa muda mrefu. “Natoa rai kwa wafanyakazi ambao tumewakabidhi nyumba hizi wazitunze, kwani Shirika limetumia fedha nyingi katika kuzikarabati,” amesema Bi. Neema. Kwa upande wao, wafanyakazi waliokabidhiw...

MRADI WA UMEME MPOMVU – GGM KUIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI GEITA – MHE. SALOME

Image
  πŸ“Œ Kukamilika kwa njia mpya kutatoa fursa kwa njia ya awali kuendelea kunufaisha  wananchi wa mkoa wa Geita na kuchochea shughuli za kiuchumi. πŸ“Œ Serikali yawekeza takribani Shilingi bilioni 63.19 kuutekeleza Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inaendelea kuimarisha miundombinu ya umeme nchini kupitia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Mpomvu hadi kituo cha kupokea na kupoza umeme cha GGM, wenye urefu wa takribani kilomita 6.7. Akizungumza Septemba 3, 2026, jijini Dodoma, wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amesema kukamilika kwa mradi huo kutaimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuchochea shughuli za kiuchumi, ikiwemo uzalishaji, ajira, ongezeko la mapato na uwekezaji. Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na TANESCO na wadau wa sekta ya nishati kuhakikisha miundombinu ya umeme inaendana na kasi ya ukuaji wa mahi...

Msajili wa Hazina, Fitch Ratings watathmini mageuzi ya taasisi za umma

Image
  Na Mwandishi wa OTR Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) Jumanne, Agosti 11, 2026, ilifanya mazungumzo na kampuni ya Fitch Ratings Ltd ikiwa ni sehemu ya mapitio ya pili ya mwaka 2026 ya tathmini ya Fitch Ratings, katika mchakato unaohusisha taasisi mbalimbali za Serikali. Mazungumzo hayo yanalenga  kuwapa wachambuzi wa Fitch Ratings fursa ya kupata taarifa za kina kuhusu mwenendo wa uchumi wa Tanzania, utekelezaji wa sera za kibajeti na fedha, pamoja na mikakati ya Serikali katika usimamizi wa deni la Taifa.  Kwa upande wa OTR, mjadala ulijikita katika utendaji wa taasisi za umma, mageuzi yanayoendelea, vihatarishi vya kifedha, pamoja na mtiririko wa fedha kati ya Serikali na taasisi za Umma. Mapema mwaka huu, Fitch Ratings iliendelea kuipa Tanzania daraja ‘B+’ kwa hadhi ya ulipaji wa madeni ya muda mrefu ya fedha za kigeni, ikitaja mwelekeo imara wa ukuaji wa uchumi na uwezo wa Serikali kukabiliana na changamoto za kifedha baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 20...

Taasisi 54 za Umma kuwasilisha taarifa za utendaji wa uwekezaji bungeni

Image
  Dodoma. Jumla ya taasisi za umma 54 zinatarajiwa kuwasilisha taarifa za utendaji wa uwekezaji mbele ya Kamati za Kudumu za Bunge kwa muda wa wiki tatu, katika mchakato unaolenga kuwezesha uchambuzi wa thamani na utendaji wa mitaji ya umma pamoja na utekelezaji wa mipango ya kimkakati ya taasisi husika. Katika awamu hii iliyoanza Jumatatu, Agosti 3, 2026, taasisi hizo zimepangwa kuwasilisha taarifa zao mbele ya Kamati mbili za Kudumu za Bunge, ambapo 27 zitawasilisha mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) na nyingine 27 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Umma (PAC). Hadi Jumatano, Agosti 5, 2026, taasisi nne zilikuwa tayari zimewasilisha taarifa zao mbele ya Kamati.  Taasisi hizo ni Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) na Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA), huku Kamati zikionesha kuridhishwa na utendaji wa taasisi husika. Uwasilish...