Posts

Showing posts from May, 2026

WAPIGA KURA 222,218 KUPIGA KURA JIMBO LA ISMANI NA KATA 12 ZA TANZANIA BARA

Image
Na Mwandishi wetu, Iringa Wapiga Kura 222,218 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura watashiriki kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Isimani lililopo Halamashauri ya Wilaya ya Iringa Mkoani Iringa na Kata 12 za Tanzania Bara.   Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele ameyasema hayo leo Mei 31, 2026 Mkoani Iringa wakati akisoma risala maalum kuhusu uchaguzi katika jimbo na kata husika utakao fanyika kesho Juni 01, 2026 na kusema kuwa jumla ya vituo 628 vya Kupigia Kura vitatumika.   “wapiga kura 89,753 wapo kwenye Jimbo la Ismani na wapiga kura 132,465 wapo kwenye kata 12 zitakazofanya uchaguzi mdogo na vituo 277 vipo kwenye Jimbo la Ismani na vituo 351 vipo kwenye kata 12 zitakazofanya uchaguzi mdogo.,”amesema Jaji Mwambegele.   Aidha, amesema Katika Uchaguzi huu, jumla ya wagombea 108 kutoka katika vyama vya siasa 17 wanawania nafasi wazi ya ubunge na udiwani katika maeneo niliyoyataja. “Jimbo la Is...

Rais Dk.Samia Apongezwa kwa Kuimarisha Vita Dhidi ya Dawa za Kulevya Nchini.

Image
  Na.Mwandishi wetu. WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera,Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu) Profesa Palamagamba Kabudi ameta taarifa ya hali ya dawa za kulevya kwa mwaka 2025 ambapo inaonesha namna Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ilivyowekeza na kuweka nguvu kubwa katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.  Akiwasilisha taarifa hiyo leo Mei 29,2029 Bungeni Mjini Dodoma ,Profesa Kabudi amesema uwasilishaji wa taarifa hiyo ni utekelezaji wa Kifungu cha 66 cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Na. 5 ya Mwaka 2015, inayoiagiza Serikali kuandaa na kuwasilisha bungeni taarifa hiyo kila mwaka. “Lengo ni kuonesha uwajibikaji wa Serikali kwa wananchi kupitia Bunge, pamoja na kutoa tathmini ya utekelezaji wa mikakati ya udhibiti wa dawa hizo kwa mwaka husika.Pia, taarifa hii inatoa nafasi kwa Bunge kutoa ushauri kwa Serikali kuhusu namna bora ya kukabiliana na tatizo la dawa za kulevya nchini.” Amefafanua kupitia Mamlaka ya Ku...

MSI Yaibua Tuzo Maalumu Kwa Wanahabari wa Afya ya Uzazi EJAT 2025

Image
  Na.Sophia Kingimali Katika hatua ya kuhamasisha uandishi wa habari unaogusa maisha ya wananchi moja kwa moja, Shirika la MSI Tanzania limezindua rasmi Tuzo ya Uandishi wa Habari za Afya ya Uzazi ndani ya Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2025. Tuzo hiyo mpya inalenga kuongeza hamasa kwa wanahabari kuandika taarifa zenye kuelimisha jamii kuhusu afya ya uzazi, huku ikitambua mchango wa vyombo vya habari katika kuleta mabadiliko ya kijamii na kiafya nchini. Akizungumza leo Mei 28, 2026 jijini Dar es salaam wakati Baraza la Habari Tanzania (MCT) likitangaza majina ya wateule wa EJAT 2025, Katibu Mtendaji wa MCT, Ernest Sungura, amesema maboresho ya tuzo hizo yanalenga kuendana na mabadiliko ya sekta ya habari na kuongeza nafasi kwa taaluma maalumu za uandishi. Mbali na tuzo ya afya ya uzazi, makundi mengine mapya yaliyoingizwa mwaka huu ni pamoja na Tuzo ya Mahojiano Bora ya Mwaka, Tuzo ya Kijana Chipukizi, Tuzo ya Uandishi wa Habari za Elimu ya Uwezo Tanzania pam...

TMA NA EMEDO KUJA NA TUZO ZA WAANDISHI WA HABARI ZENYE LENGO LA KUHAMASISHA ELIMU YA HALI YA HEWA.

Image
Na.Mwandishi wetu. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO) leo imetangaza rasmi ushirikiano wa Tuzo za Waandishi wa Habari zinazolenga kuhamasisha kutambua mchango wa vyombo vya habari katika kuelimisha jamii kuhusu changamoto za matukio ya hali mbaya ya hewa, na utoaji wa tahadhari za mapema, na usalama kwenye maji hapa Tanzania. Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika , Jijini Dar -Es -Salaam, Bi. Mary Francis Mahemba, Afisa Uchechemuzi (Advocacy Officer) kutoka Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo - EMEDO alisema kuwa vyombo vya habari vina nafasi muhimu katika kuifikia jamii kwa taarifa sahihi zinazoweza kusaidia kuokoa maisha, kupunguza athari za majanga yanayohusiana na hali ya hewa,pamoja na kuimarisha uelewa wa jamii kuhusu usalama majini. “Waandishi wa habari ni wadau muhimu katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu tahadhari za hali ya he...

JAJI MWAMBEGELE AWAPA NENO MAKARANI WA UCHAGUZI ISIMANI

Image
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa    Mhe.Jacobs Mwambegele akizungumza wakati alipotembelea mafunzo ya siku moja kwa Makarani  waogozaji Wapiga Kura katika Jimbo la Isimani yaliyofanyika katika Shule Sekondari Ufundi Ifunda mkoani Iringa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi huo utakaofanyika Jumatatu ya Juni 1, 2026. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa    Mhe.Jacobs Mwambegele akizungumza wakati alipotembelea mafunzo ya siku moja kwa Makarani  waogozaji Wapiga Kura katika Jimbo la Isimani yaliyofanyika katika Shule Sekondari Ufundi Ifunda mkoani Iringa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi huo utakaofanyika Jumatatu ya Juni 1, 2026. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa    Mhe.Jacobs Mwambegele amewataka watendaji wa uchaguzi ambao ni Makarani waongozaji Wapiga kura kufanya kazi yao kwa kufuata Sheria, Kanuni na utarat...

WANAHABARI WATAKIWA KUJIUNGA VYAMA VYA WAFANYAKAZI KULINDA HAKI ZAO

Image
  Na.Sophia Kingimali. Rais wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA), Tumaini Nyamhokya, amewataka wanahabari nchini kujiunga na vyama vya wafanyakazi ili kujenga umoja, kulinda maslahi yao na kupigania haki zao mahali pa kazi kwani kupitia umoja huo waandishi wa habari wataweza kupata nguvu ya pamoja katika kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ukosefu wa mikataba ya ajira na mazingira magumu ya kazi. Akizungumza leo Mei 25 katika mafunzo yaliyoandaliwa kwa kushirikiana kati ya JOWUTA na Mfuko wa fidia kwa wafanyakazi  (WCF), Nyamhokya amesema vyama vya wafanyakazi vina mchango mkubwa katika kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki zao na kutetea maslahi yao wanapokumbwa na changamoto kazini. Alisema waandishi wengi wa habari wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu bila mikataba rasmi ya ajira huku wengine wakilipwa kwa kutegemea idadi ya habari wanazoandika, hali ambayo inawanyima uhakika wa maisha na mafao muhimu ya kazi. Aidha Nyamhok...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yatoa wito wa utawala bora kuimarisha uwekezaji wa umma

Image
  Zanzibar.  Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) imesisitiza kuwa mustakabali wa mafanikio ya taasisi na mashirika ya umma nchini unategemea kwa kiwango kikubwa uimara wa mifumo ya utawala bora, uwajibikaji na uongozi wenye maono yanayolenga matokeo. Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Chacha Marigiri, alipowasilisha mada kuhusu ‘Utawala bora katika mashirika ya Umma na Majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Hazina’ katika Mkutano wa Jukwaa la Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma Zanzibar uliofanyika katika hoteli ya Golden Tulip Airport. Katika wasilisho lake Jumapili, Mei 24, 2026, Bw. Marigiri alisema kuwa kasi ya kufikia maendeleo endelevu haiwezi kupatikana kwa uwekezaji pekee, bali kupitia mifumo imara ya usimamizi inayohakikisha rasilimali za umma zinalindwa na kuzalisha kwa maendeleo ya Taifa. Alisema thamani ya uwekezaji wa Serikali katika taasisi za umma na kampuni ambazo Serikali ina hisa chache kwa sas...

BRELA YAWEKA MKAZO URASIMISHAJI BIASHARA JIJINI MBEYA

Image
  Na.Mwandishi wetu. Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umewataka wadau na wafanyabiashara wa nyanda za juu kusini hususan katika jiji la Mbeya, kuchangamkia fursa za urasimishaji wa biashara ili kuingia kwenye mfumo rasmi wa kiuchumi unaotambulika kisheria utakaowasaidia kuhimili ushindani wa soko la ndani na kimataifa. Wito huo umetolewa tarehe 22 Mei, 2026 na Msaidizi wa Usajili Mkuu kutoka BRELA, Bi. Hellen Mhina wakati wa maonyesho ya biashara na uwekezaji ya Mbeya City Expo 2026 yanayoendelea jijini humo huku akieleza kuwa urasimishaji ni nguzo kuu inayomlinda mfanyabiashara na kumpa fursa ya kukua kiushindani. Akizungumza ushiriki wa BRELA katika maonyesho hayo, Bi. Mhina alieleza kuwa huo ni muendelezo wa mkakati wa Wakala kufikisha elimu ya urasimishaji biashara kwa watu wengi ambapo kwa sasa huduma za usajili wa Jina la Biashara, Leseni ya Biashara na Leseni ya Kiwanda zinapatika kwenye mfumo ulioboreshwa wa BRELA Online Services (BOS) ambao ni rahisi zaidi k...

TARURA YAWAIMARISHA MAAFISA UNUNUZI KUDHIBITI HOJA ZA UKAGUZI ‎

Image
  ‎Morogoro ‎ ‎Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imewahimiza Maafisa Ununuzi kuzingatia kikamilifu sheria, kanuni na taratibu za ununuzi ili kudhibiti upotevu wa fedha za serikali na kuondoa hoja za ukaguzi zinazojitokeza mara kwa mara katika utekelezaji wa miradi. ‎ ‎Kauli hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff wakati akifunga mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Vitengo vya Ununuzi TARURA kutoka mikoa yote 26 yaliyofanyika mkoani Morogoro. ‎ ‎Mhandisi Seff alisema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wataalamu wa ununuzi kuhusu utekelezaji sahihi wa sheria ya ununuzi pamoja na namna ya kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo katika majukumu yao ya kila siku. ‎ ‎Alisema moja ya changamoto kubwa zinazojitokeza ni kuchaguliwa kwa wakandarasi wasio na uwezo wa kutekeleza miradi kwa ufanisi pamoja na udhaifu katika usimamizi wa dhamana mbalimbali za mikataba, hususan dhamana za malipo ya awali. ‎ ‎"Tumekuwa tukiona changamo...

MKURUGENZI WA RASILIMALI WATU TANESCO AWAHAKIKISHIA USHIRIKIANO MAAFISA HUDUMA KWA WATEJA KUBORESHA UTENDAJI

Image
  📌 Afunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa hao 📌 Awapongeza kwa utendaji bora wenye kujenga taswira chanya ya Serikali na Shirika kwa wananchi Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala TANESCO, Bi. Beatrice Kimoleta, amewahakikishia Maafisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja ushirikiano katika kufanikisha upatikanaji wa nyenzo muhimu zitakazowawezesha kuhudumia wateja kwa ufanisi na ubora wa hali ya juu. Ametoa kauli hiyo Mei 22, 2026 alipokuwa akifunga mkutano mkuu wa mwaka wa maafisa hao uliofanyika kwa siku tano kuanzia Mei 18, 2026  jijini Dodoma, mkutano ambao hufanyika kila mwaka kwa lengo la kufanya tathmini ya kuboresha utendaji kazi wa kurugenzi ili kufanikisha malengo yaliyowekwa. “Kwa uongozi wa Shirika, kipaumbele chetu ni kuhakikisha watumishi wanaohudumia wateja moja kwa moja wanakuwa katika mazingira mazuri ya kazi ili waweze kutoa huduma kwa ufanisi. Tunawahakikishia kuwapatia nyenzo muhimu ili muendelee kutoa huduma bora kwa wateja,” ameeleza , Bi. Kimoleta . Ame...

BANDARI YA MBAMBA BAY KUFUNGUA FURSA MPYA ZA BIASHARA YA MAFUTA UKANDA WA KUSINI

Image
  Na Mwandishi Wetu Ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay unatarajiwa kuchochea kwa kiasi kikubwa biashara ya mafuta katika ukanda wa Kusini na kufungua njia mpya za usafirishaji wa bidhaa hiyo kuelekea nchi jirani kupitia miundombinu ya kisasa inayojengwa eneo hilo. Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bandari hiyo, Meneja wa Mipango ya Mafuta wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Gilbert Jungulu, amesema mradi huo una nafasi ya kuifanya Tanzania kuwa kitovu muhimu cha usambazaji wa mafuta kwa nchi za Malawi, Msumbiji na maeneo mengine ya ukanda huo. Amesema PBPA itaendelea kuratibu uagizaji wa mafuta nchini pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha miundombinu muhimu ya mafuta, ikiwemo maghala ya kuhifadhia mafuta, inajengwa na kuimarishwa ili kurahisisha biashara ya kikanda. “Endapo maghala ya kuhifadhia mafuta yatakamilika hapa Mbamba Bay, itakuwa rahisi meli kushusha mafuta kwa ajili ya kuhifadhiwa na baadaye kusafirishwa kwenda nchi j...

SALOME: NGUZO ZA ZEGE NA CHUMA KUTUMIKA KUKABILI CHANGAMOTO YA KUANGUKA KWA NGUZO ZA UMEME ZA MITI.

Image
  Na.Mwandishi wetu. NAIBU Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba amesema Serikali kupitia TANESCO inaendelea kubadilisha nguzo chakavu kwa kuweka nguzo imara zaidi, zikiwemo nguzo za zege na chuma, pamoja na kuimarisha misingi ya nguzo katika maeneo yenye udongo laini ili kukabili changamoto ya kuanguka kwa nguzo za umeme. Salome ameeleza hayo leo, Mei 22, 2026, Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Sara Msafiri Ally, Mbunge wa Mvomero, aliyetaka kujua ni lini Serikali itatatua changamoto ya kuanguka kwa nguzo za umeme katika Tarafa ya Mgeta. Akijibu swali hilo, Salome amesema Serikali inatambua uwepo wa changamoto ya kuanguka kwa nguzo za umeme katika baadhi ya maeneo ya Tarafa ya Mgeta kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo mvua nyingi, uwepo wa udongo usiohimilivu pamoja na uchakavu wa baadhi ya nguzo. Amesema Serikali kupitia TANESCO inaendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa miundombinu ya umeme ili kubaini na kushughulikia changamoto hizo mapema pindi zinapo...

MD TWANGE AELEZA KUTORIDHISHWA NA KASI YA MKANDARASI WA MRADI WA HALE

Image
  📍Ni ule wa kuboresha kituo cha kufua umeme  📍Amuagiza kuongeza kasi ya utekelezaji wa Mradi huo Na Mwandishi Wetu, Korogwe, Tanga Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bw. Lazaro Twange ameeleza kutoridhishwa na kasi ya mkandarasi anayetekeleza mradi wa maboresho ya Kituo cha Kufua Umeme cha Hale kutokana na kuchelewa kukamilika kwa Mradi huo ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2022. Bw. Twange ameyasema hayo leo Mei 22, 2026 wakati wa ziara yake ya ukaguzi katika mradi wa Hale pamoja na mradi wa usafishaji wa bwawa la Mto Pangani iliyopo katika Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga ambapo amemtaka mkandarasi wa Mradi wa Hale kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo ikiwa ni pamoja na kuongeza wafanyakazi pamoja na muda wa kufanya kazi ili ukamilike kwa wakati. “Siridhishwi sana na mwenendo wake. Mkandarasi amewahi kuomba nyongeza ya muda mara mbili na nimepata taarifa kuwa yuko kwenye hatua za kuomba nyongeza nyingine ya tatu. Ndio maana nimekuja kuona kuna nini,” amesema Bw. Twange. Ame...