Posts

Showing posts from August, 2026

Msajili wa Hazina, Fitch Ratings watathmini mageuzi ya taasisi za umma

Image
  Na Mwandishi wa OTR Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) Jumanne, Agosti 11, 2026, ilifanya mazungumzo na kampuni ya Fitch Ratings Ltd ikiwa ni sehemu ya mapitio ya pili ya mwaka 2026 ya tathmini ya Fitch Ratings, katika mchakato unaohusisha taasisi mbalimbali za Serikali. Mazungumzo hayo yanalenga  kuwapa wachambuzi wa Fitch Ratings fursa ya kupata taarifa za kina kuhusu mwenendo wa uchumi wa Tanzania, utekelezaji wa sera za kibajeti na fedha, pamoja na mikakati ya Serikali katika usimamizi wa deni la Taifa.  Kwa upande wa OTR, mjadala ulijikita katika utendaji wa taasisi za umma, mageuzi yanayoendelea, vihatarishi vya kifedha, pamoja na mtiririko wa fedha kati ya Serikali na taasisi za Umma. Mapema mwaka huu, Fitch Ratings iliendelea kuipa Tanzania daraja ‘B+’ kwa hadhi ya ulipaji wa madeni ya muda mrefu ya fedha za kigeni, ikitaja mwelekeo imara wa ukuaji wa uchumi na uwezo wa Serikali kukabiliana na changamoto za kifedha baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 20...

Taasisi 54 za Umma kuwasilisha taarifa za utendaji wa uwekezaji bungeni

Image
  Dodoma. Jumla ya taasisi za umma 54 zinatarajiwa kuwasilisha taarifa za utendaji wa uwekezaji mbele ya Kamati za Kudumu za Bunge kwa muda wa wiki tatu, katika mchakato unaolenga kuwezesha uchambuzi wa thamani na utendaji wa mitaji ya umma pamoja na utekelezaji wa mipango ya kimkakati ya taasisi husika. Katika awamu hii iliyoanza Jumatatu, Agosti 3, 2026, taasisi hizo zimepangwa kuwasilisha taarifa zao mbele ya Kamati mbili za Kudumu za Bunge, ambapo 27 zitawasilisha mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) na nyingine 27 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Umma (PAC). Hadi Jumatano, Agosti 5, 2026, taasisi nne zilikuwa tayari zimewasilisha taarifa zao mbele ya Kamati.  Taasisi hizo ni Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) na Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA), huku Kamati zikionesha kuridhishwa na utendaji wa taasisi husika. Uwasilish...

KITUO CHA UBIA CHAKUTANA NA WANAHABARI KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS.

Image
  • Ni katika kusukuma mkakati wa uchumi wa Dola trilioni moja Na Mwandishi Wetu. DAR ES SALAAM. Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC), David Kafulila, ameanza kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukutana na waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii ili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050. Kikao hicho cha kimkakati kilichofanyika Jumanne, Agosti 4, 2026, katika ofisi za PPPC jijini Dar es Salaam. Kafulila amekutana na waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii siku moja baada ya Rais Samia kutangaza, wakati wa uzinduzi wa nyenzo za utekelezaji wa Dira 2050 uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam, kuwa nchi sasa inaingia katika hatua ya utekelezaji wa vitendo na kwamba muda wa maneno umekwisha. Katika kikao hicho, Kafulila amesema hatua ya kukutana na wamiliki na waandishi wa majukwaa ya kidijitali inalenga kutekeleza agizo la moja kwa moja la Rais Samia, aliyezitaka taasisi za umma kutoa elimu kwa wana...