Posts

Showing posts from June, 2026

WAZIRI MKUU AMPONGEZA KAFULILA, ASEMA NI KIONGOZI KIJANA MWENYE UPEO MPANA

Image
  Amtaja Kama Kiongozi Kijana Mwenye Exposure ya Kimataifa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwigulu Nchemba, amemsifu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP Centre), David Kafulila, akimtaja kuwa ni miongoni mwa viongozi vijana wenye uwezo wa kuelewa mwenendo wa maendeleo duniani na kutumia uzoefu huo kusukuma mageuzi nchini. Akizungumza leo Jumanne, Juni 30, 2026, wakati wa Uzinduzi wa Mfumo wa Tanzania Chamber Portal na Mkutano wa Mwaka wa Biashara na Uwekezaji 2026, Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwaamini vijana katika nafasi za uongozi kutokana na uwezo wao wa kuleta matokeo. Amemtaja Kafulila kama mfano wa viongozi hao, akisema ana upeo mpana wa masuala ya maendeleo na hufuatilia mifumo iliyofanikiwa katika nchi mbalimbali ili kuitafsiri katika mazingira ya Tanzania. "Kwa bahati nzuri sana Rais Samia ameamini vijana katika kila eneo. Ukienda P...

HALOTEL yaleta teknolojia za kisasa sabasaba,yasukuma mageuzi ya kidigital

Image
  Na Mwandishi Wetu Kampuni ya mawasiliano ya Halotel Tanzania imezindua rasmi ushiriki wake katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), maarufu kama SabaSaba, kwa kuwasogezea wananchi huduma za kisasa za mawasiliano na kifedha zinazolenga kuharakisha mageuzi ya kidigitali nchini. Ikiwa na kauli mbiu ya "Teknolojia kutoka Moyoni," Halotel imesema maonesho hayo ni fursa ya kuwaonesha wananchi na wadau suluhisho mbalimbali za kidigitali zinazorahisisha maisha ya kila siku na kusaidia ukuaji wa uchumi. Pia,Wageni wanaotembelea banda la kampuni hiyo wanapata nafasi ya kujionea huduma za mtandao wa 5G, intaneti ya kasi ya juu ya HaloFibre, suluhisho za kidigitali kwa biashara pamoja na huduma za kifedha kupitia HaloPesa. Akizungumza katika uzinduzi wa banda hilo leo Juni,2026 kwenye maonesho ya 50 ya kimataifa ya biashara,Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Halotel Tanzania, Bw. Abdallah Salum, alisema maonesho ya SabaSaba yanatoa nafasi ya kampuni hi...

KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UZALISHAJI UMEME KITUO CHA JULIUS NYERERE.

Image
   ðŸ“ŒYasema Kituo kinachangia asilimia 45 ya umeme katika Gridi ya Taifa. 📌Yasisitiza ukamilishaji wa miradi ya njia za kusafirisha umeme ili kuwafikia wananchi.  Yawapongeza wananchi kwa kuchangia ujenzi wa Kituo hicho kupitia kodi zao. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imesema imeridhishwa na maendeleo ya uzalishaji wa umeme katika Kituo cha Kufua Umeme cha Julius Nyerere, ambacho kwa sasa kinachangia asilimia 45 ya umeme unaoingia katika Gridi ya Taifa. Akizungumza leo, Juni 29, 2026, mara baada ya kutembelea Kituo hicho, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Subira Mgalu, amesema Kamati imejionea kazi kubwa na ya kihistoria iliyofanyika katika ujenzi wa Kituo hicho pamoja na mchango wake mkubwa katika kuhakikisha Taifa linapata nishati ya umeme ya uhakika. Mhe. Mgalu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuhakikisha Kituo hicho ambacho ni cha pili kwa ukubwa barani Afrika kwa uzalishaji wa umeme kinakamilika na...

Msajili wa Hazina aonya taasisi za umma zenye utendaji duni.

Image
  Dar es Salaam. Serikali imeonya taasisi za umma zinazofanya vibaya kujitathmini na kuchukua hatua za haraka za kuboresha utendaji wao, ikisisitiza kuwa haitavumilia taasisi zitakazoendelea kuonesha utendaji duni kwa muda mrefu. Onyo hilo lilitolewa na Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, jijini Dar es Salaam Ijumaa, Juni 26, 2026, wakati wa mahojiano maalumu kuelekea Siku ya Gawio itakayofanyika Jumanne, Juni 30, 2026, katika Ikulu ya Dar es Salaam. Bw. Mchechu alisema taasisi zote zinazostahili kuwasilisha gawio na michango mingine Serikalini zinapaswa kutekeleza wajibu huo kwa wakati, akisisitiza kuwa kushindwa kufanya hivyo ni kuinyima Serikali na wananchi mapato stahiki. “Mashirika si mali ya bodi za wakurugenzi wala menejimenti; ni mali ya umma zinazosimamiwa na Serikali. Kwa muktadha huo, kurejesha kilicho haki ya wananchi si fadhila, bali ni wajibu,” alionya. Alisisitiza kuwa viongozi wa taasisi za umma wanapaswa kuhakikisha malengo ya faida wanayopewa yanafikiwa ili k...

MD TWANGE afafanua chanzo cha hitilafu iliyotokea kwenye gridi ya umeme ya Taifa.

Image
📌 Aomba radhi kwa wateja wananchi na kuwahakikishia upatikanaji endelevu wa huduma ya umeme  📌 Asema uzalishaji wa umeme umefikia megawati 4400 na juhudi za kuimarisha Mfumo wa Gridi zinaendelea Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. Lazaro Twange, leo amewaomba radhi wananchi na wateja wote wa huduma ya umeme kufuatia hitilafu iliyojitokeza kwenye Mfumo wa Gridi ya Umeme ya Taifa siku ya jana Juni 27, 2026, iliyosababisha kukosekana kwa huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali nchini. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 28, 2026, Bw. Twange amesema uchunguzi wa awali uliofanywa wakati wa hatua za kurejesha huduma umebaini kuwa kutoka kwa Gridi kulisababishwa na hitilafu zilizojitokeza kwa wakati mmoja katika njia tatu za usafirishaji wa umeme pamoja na mashine moja ya kuzalisha umeme. Ameeleza kuwa , Gridi ya Umeme ya Taifa ni mfumo mmoja unaounganisha miundombinu ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa umeme, hivyo hiti...

MHE. SALOME AHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KUPITIA MARATHON

Image
  Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, leo Juni 27, 2026 ameshiriki Mbio za Nishati Safi ya Kupikia (Clean Cooking Marathon) zilizofanyika katika Viwanja vya St. Peters Oysterbay jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini. Akizungumza wakati wa kufungua mbio hizo, Mhe. Salome amesema pamoja na hatua nzuri iliyofikiwa, matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini bado yako katika kiwango cha asilimia 28.6, hali inayoonesha kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kufikia lengo la asilimia 80 ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034. Amesema mbio hizo si mashindano ya kawaida ya kutafuta medali au vikombe, bali ni chachu ya mabadiliko ya kifikra na kijamii yanayolenga kulinda afya za wananchi, kuhifadhi mazingira na kuwawezesha wananchi kiuchumi, huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia wa mwaka 2024–2034 unaolenga kuha...

KATIBU MKUU WA NISHATI ZAMBIA AIPONGEZA TANZANIA KWA MAFANIKIO MAKUBWA KATIKA SEKTA YA UMEME

Image
  📌Aeleza Ushirikiano katika utekelezaji wa Mradi wa TAZA na faida zake Kikanda  📌Asifu jitihada za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati nchini Zambia,  Mhe. Arnold Simwaba, amesema kuwa Tanzania na Zambia zimeendelea kushirikiana katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa TAZA (Tanzania–Zambia Power Interconnection Project), wenye lengo la kuunganisha gridi za umeme za nchi hizo mbili kwa manufaa ya pande zote. Mhe. Simwaba ameyasema hayo Juni 25, 2026, mkoani Dodoma, wakati wa kikao cha pamoja kilichowakutanisha wajumbe kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wizara ya Nishati ya Zambia, Mamlaka ya Umeme Vijijini ya Zambia pamoja na Shirika la Umeme Zambia (ZESCO), kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kujadili namna ya kuboresha huduma za umeme. Ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kubwa katika sekta ya umeme baada ya miradi mingi ya umeme kukamilika nchini. Aidha...

Mzumbe yajipanga kutafiti fursa za uwekezaji kupitia PPP

Image
  Na.Mwandishi wetu,Morogoro. Chuo Kikuu cha Mzumbe kimesema kitafanya tafiti za kina kubaini maeneo yenye fursa za uwekezaji kupitia ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPP), hatua inayolenga kuisaidia Serikali kufanya maamuzi ya uwekezaji yanayozingatia ushahidi wa kisayansi. Hatua hiyo pia inalenga kuimarisha mchango wa chuo katika maendeleo ya taifa kupitia tafiti, mafunzo na ushauri wa kitaalamu kuhusu utekelezaji wa miradi ya ubia. Akizungumza wakati wa mhadhara  ya kujenga uwezo kuhusu PPP yaliyofanyika chuoni hapo, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi Profesa Hawa Tundui amesema Mzumbe imechagua PPP kuwa moja ya maeneo ya kimkakati ya utafiti kutokana na mchango wake katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi. "Tunataka kufanya tafiti zitakazotusaidia kubaini fursa zilizopo katika eneo la PPP na kuishauri Serikali kuhusu maeneo yanayohitaji kupewa kipaumbele. Hili ni eneo jipya lenye fursa nyingi, hivyo kama wanataaluma tu...

Bidhaa bandia zatajwa kutishia afya,uchumi na biashara halali

Image
  Na Mwandishi Wetu Serikali imezitaka taasisi zote zinazohusika na udhibiti wa bidhaa nchini kuimarisha mapambano dhidi ya bidhaa bandia, hususan pombe, vilainishi na sigara bandia, ambazo zimeendelea kuhatarisha afya za wananchi, kuathiri biashara halali na kupunguza mapato ya Serikali. Kauli hiyo imetolewa leo Juni 25,2026 na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam katika kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kudhibiti Bidhaa Bandia Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam chini ya kaulimbiu isemayo “Linda maisha na masoko dhidi ya pombe, vilainishi na sigara bandia.” Mapunda amesema biashara ya bidhaa bandia imekuwa changamoto kubwa inayohitaji ushirikiano wa wadau wote kutokana na athari zake kwa afya za wananchi, mazingira ya biashara na uchumi wa taifa kwa ujumla. Ameeleza kuwa licha ya juhudi zinazofanywa na Tume ya Ushindani (FCC), bado kuna haja ya kuongeza matumizi ya teknolojia za kisasa katika uchunguzi, ufuatilia...

BRELA YAVUNJA REKODI YA MAFANIKIO 2025/2026, YAAINISHA MATARAJIO YAKE 2026/27

Image
    NA MWANDISHI WETU Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imezidi kujipambanua kama muhimili na nguzo madhubuti katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa, kupitia mikakati yake endelevu inayolenga kurasimisha shughuli za kiuchumi na kuhakikisha kuwa hakuna Mtanzania anayeachwa nyuma katika upatikanaji wa huduma za sajili na leseni. Hayo yamebainishwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa, wakati akifungua kikao kazi cha wafanyakazi wa Wakala hiyo kilichofanyika mkoani Morogoro tarehe 20 Juni 2026. “Katika mwaka wa fedha wa 2025/2026, BRELA imefanikiwa kuvuka malengo na kutekeleza majukumu yake ya msingi kwa ufanisi mkubwa ikijikita katika kuboresha huduma kwa wadau, kuimarisha mifumo ya kidijitali, na kupanua wigo wa urasimishaji biashara nchini licha ya changamoto mbalimbali za kimazingira na kiuchumi zilizojitokeza” Alisema Bw. Nyaisa Aidha, Kaimu Meneja wa Sehemu ya Mipango, Utafiti na Ubunifu wa BRELA, Bi. Alinda Lema, alibainisha kuwa mafanikio ...

AFRIKA yaonywa kuhusu janga la magonjwa yasiyoambukiza.

Image
Na Sophia Kingimali, Dar es Salaam Magonjwa yasiyoambukiza (NCDs) yameendelea kuwa tishio kubwa kwa afya na uchumi wa nchi za Afrika, hali iliyochochea viongozi wa afya kutoa wito wa kuongeza uwekezaji katika kinga, matibabu na kuimarisha mifumo ya huduma za afya ili kuokoa maisha ya mamilioni ya wananchi. Wito huo umetolewa leo juni 23,2026 katika Mkutano wa Tatu wa Kimataifa wa PEN-Plus Afrika 2026 unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, ambapo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Waziri wa Afya Mohamed Mchengerwa, alizitaka nchi za Afrika kuweka afya kuwa ajenda ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Akifungua mkutano huo kwa niaba ya Rais Samia, Mchengerwa alisema magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari, shinikizo la damu, saratani, magonjwa ya moyo, selimundu na changamoto za afya ya akili yamekuwa mzigo mkubwa kwa mataifa ya Afrika na yanahitaji hatua za pamoja za kuyadhibiti. Alisema kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani...

JKT Yafunga Rasmi Mashindano ya CNS Cup 2026, Yasisitiza Nidhamu na Kukuza Vipaji.

Image
  Na.Mwandishi wetu. Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limefunga rasmi Mashindano ya Kombe la CNS Cup 2026 katika Kambi ya JKT Mgulani jijini Dar es Salaam, huku likisisitiza umuhimu wa michezo katika kuimarisha nidhamu, uzalendo, afya na kuibua vipaji vya vijana wanaojitolea kulitumikia taifa kupitia jeshi hilo. Akifunga mashindano hayo kwa niaba ya Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele, Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo JKT, Brigedia Jenerali Peter Mnyani,amesema michezo imeendelea kuwa sehemu muhimu ya mafunzo ya JKT kwa kuwa inajenga uwezo wa kimwili na kiakili, huku ikiwajengea vijana nidhamu, moyo wa kujituma, uongozi na mshikamano unaohitajika katika utendaji wa majukumu ya kijeshi. Amesema mashindano ya CNS Cup yameendelea kuwa jukwaa muhimu la kutambua na kuendeleza vipaji vya wanamichezo kutoka vikosi mbalimbali vya JKT, ambao baadaye hujiunga na timu teule za jeshi hilo kushiriki mashindano ya kijeshi na kitaifa. "Michezo ni ajira na ni fursa ya maendeleo kwa vijana. Wale waliop...

MADIWANI WA MPANDA NA NSIMBO WAIPONGEZA SERIKALI KWA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA KITUO CHA KUFUA UMEME CHA JULIUS NYERERE.

Image
  Na Mwandishi wetu, Rufiji - Pwani Madiwani wa Halmashauri za Wilaya za Mpanda na Nsimbo mkoani Katavi, wakiongozana na baadhi ya wabunge na viongozi wengine, wamepongeza uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika Kituo cha Kufua Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP) baada ya kujionea kwa karibu uendeshaji wa kituo hicho na mchango wake katika maendeleo ya sekta ya nishati nchini. Viongozi hao walitembelea kituo hicho tarehe 20 Juni 2026 kwa lengo la kujionea uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali, kufahamu namna kituo kinavyoendeshwa pamoja na kupata uelewa wa mchango wake katika kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini. Ziara hiyo ilihusisha madiwani 22 pamoja na baadhi ya wabunge na viongozi wengine kutoka Mkoa wa Katavi. Akizungumza baada ya ziara hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda, Charles Philipo, aliishukuru Serikali kwa juhudi kubwa inazoendelea kufanya katika kuimarisha sekta ya nishati na kuipongeza TANESCO kwa kuwapatia viongozi hao fursa ya kujionea kituo hicho. “...

WAZIRI NDEJEMBI: WAKANDARASI WA UMEME WASIOFANYA VIZURI WASIPEWE MIRADI MINGINE

Image
  📌*Apongeza mchango REA katika kufikisha asilimia 78.1 ya upatikanaji umeme vijijini* 📌*Apongeza wakandarasi wazawa waliofanya vizuri katika utekelezaji wa miradi; Ataka wapewe kazi zaidi* Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameuelekeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha kuwa wakandarasi ambao hawajafanya vizuri katika utekelezaji wa miradi ya umeme inayosimamiwa na Wakala huo  kutopewa  kazi nyingine, ili kutokwamisha lengo la Serikali la kuwafikishia wananchi huduma ya umeme kwa wakati na kwa ufanisi. Mhe. Ndejembi ametoa maelekezo hayo tarehe 22 Juni, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakandarasi wa miradi ya umeme pamoja na wadau wa miradi ya nishati vijijini.  Kikao hicho kilienda sambamba na utoaji wa tuzo kwa wakandarasi waliofanya vizuri katika utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini na vitongojini, ikiwemo waliokamilisha kazi mapema kabla ya muda wa mwisho wa mikataba yao. "Umeme sasa ...