Posts

Showing posts from July, 2026

Taasisi za Umma zatakiwa kutokuwa kikwazo kwa wawekezaji

Image
Na Mwandishi wa OTR Pwani. Serikali imezitaka Taasisi za Umma kuhakikisha zinakuwa chachu ya ukuaji wa uchumi kwa kutengeneza mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji kupitia mifumo yenye ufanisi, kupunguza urasimu usio wa lazima, kuboresha utoaji wa huduma na kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi katika kuunga mkono utekelezaji wa Dira 2050. Wito huo ulitolewa Julai 24,2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, wakati akifunga awamu ya tatu ya Programu ya Mafunzo Elekezi ya siku nne kwa Watendaji Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha mkoani Pwani. Akizungumza na viongozi hao, Mhe. Kikwete alisema mafanikio ya Dira 2050 hayatategemea ubora wa sera na mipango pekee, bali namna taasisi za umma zitakavyotekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuzalisha matokeo yanayoonekana kwa wananchi na kwa uchumi wa Taifa. Amewataka Wakuu wa Taasisi za Umma ku...

Taasisi za umma zatakiwa kuachana na utendaji wa mazoea ili kufanikisha Dira 2050

Image
  Na Mwandishi wa OTR Pwani. Serikali imezitaka Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali kuachana na utendaji wa mazoea na kujielekeza katika uongozi unaozingatia matokeo, ubunifu, uwajibikaji na ushirikiano wa karibu na sekta binafsi ili kuharakisha utekelezaji wa DIRA ya Taifa ya Maendeleo 2050. Wito huo ulitolewa Jumanne jioni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, wakati akifungua Mafunzo Elekezi kwa Watendaji Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali yanayoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Taasisi ya UONGOZI katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha mkoani Pwani. Mafunzo hayo ya siku nne yanafanyika chini ya kaulimbiu "Kutoka Maono mpaka Matokeo: Kufungamanisha Utendaji wa Mashirika ya Umma na DIRA 2050."   Akizungumza katika hafla hiyo, Prof. Mkumbo alisema Tanzania imeweka lengo la kufikia uchumi wa kati wa juu na kukuza Pato la Taifa (GDP) kutoka dola za Ma...

WAZIRI NDEJEMBI ATOA ONYO KWA MKANDARASI ANAYETEKELEZA MRADI WA SONGEA–TUNDURU–MASASI

Image
  📌 Asema ucheleweshaji wa mradi hauendani na matarajio ya Serikali na wananchi. 📌 Amuagiza mkandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji na kuzingatia masharti ya mkataba. 📌 Aelekeza hatua stahiki kuchukuliwa iwapo maendeleo ya mradi hayataboreshwa kabla ya Septemba 30, 2026. 📌 Mradi wa kV 220 utaiunganisha Mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye Gridi ya Taifa na kuimarisha upatikanaji wa umeme Kusini mwa Tanzania. 📍Tunduru, Ruvuma  Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameonesha kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Songea hadi Masasi kupitia Tunduru na kuagiza mkandarasi kuongeza juhudi ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati uliopangwa. Akizungumza wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo leo Julai 22, 2026, Mhe. Ndejembi amesema Serikali haitakuwa tayari kuona miradi ya kimkakati inayogusa maisha ya wananchi ikicheleweshwa bila sababu za msingi. Amesema mradi huo ni miongoni mwa miradi muhimu...

NEWALA KUNUFAIKA NA UMEME WA UHAKIKA.

Image
  📌*Ni baada ya kukamilika kwa njia ya kusafirisha umeme ya kilovoti 33 Masasi - Mtwara* 📌*Mradi umeimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi wa Wilaya ya Newala na maeneo jirani.* 📌*MD Twange asema thamani ya mradi ni takribani shilingi bilioni 4.65* 📍Newala, Mtwara | Julai 21, 2026 Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amezindua rasmi mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 33 kutoka Masasi hadi Newala, akieleza kuwa mradi huo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuendelea kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi na kuweka mazingira wezeshi kwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika Wilaya ya Newala. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa njia hiyo, Mhe. Ndejembi amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuwekeza katika miradi ya kimkakati ya umeme ili kuhakikisha huduma ya nishati inawafikia wananchi wengi zaidi na kuwa chachu ya maendel...

SUA yaipongeza PPPC kwa kukuza ajenda ya ubia katika sekta ya kilimo

Image
  Na.Mwandishi wetu.  Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimepongeza Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta ya Binafsi (PPPC) kwa kuendelea kuhamasisha matumizi ya ubia (PPP) kama nyenzo ya kuharakisha maendeleo ya sekta ya kilimo na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa. Akizungumza leo July 17,2026 wakati wa Mhadhara wa Wazi kwa Umma ulioandaliwa na PPPC katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Naibu Makamu Mkuu wa SUA, Prof. Amandus Muhairwa, alisema uamuzi wa PPPC kuandaa mhadhara huo chuoni hapo unaonesha kutambua nafasi ya kimkakati ya kilimo katika kufanikisha ajenda ya maendeleo ya Tanzania. Alisema SUA imefarijika kuwa miongoni mwa taasisi za elimu ya juu zinazoshirikishwa katika mijadala kuhusu ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, akibainisha kuwa ushirikiano huo ni hatua muhimu katika kuunganisha elimu, utafiti, ubunifu na uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya Taifa. "Tunayo heshima kubwa kumpokea Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC, Bw. David Kafulila, pam...

Tanzania imeitaka WIPO kujenga mfumo jumuishi wa miliki ubunifu ili nchi zinazoendelea zinufaike na akili mnemba*

Image
  Geneva, Julai 2026  Tanzania imelitaka Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) kujenga mfumo wa kimataifa wa miliki bunifu unaowezesha nchi zinazoendelea kunufaika na maendeleo ya akili mnemba (Artificial Intelligence–AI), huku ikisisitiza umuhimu wa kuhamasisha matumizi ya teknolojia na kujengea watu uwezo. Akiwasilisha taarifa ya nchi kwa niaba ya Mhe Balozi Possi katika Mkutano wa 68 wa Nchi Wanachama wa Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) ulioanza tarehe 7 Julai, 2026 na kufanyika Geneva Uswisi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Hoyce Temu, alisema miliki ubunifu imekuwa nyenzo muhimu ya kukuza ubunifu, viwanda na maendeleo ya uchumi. "Tanzania inatambua miliki ubunifu kama kichocheo cha kimkakati cha ubunifu, uvumbuzi wa teknolojia, maendeleo ya viwanda na maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi," alisema. Alisema Tanzania inaendelea kujenga uchumi unaotegemea maarifa na inaiona akili mnemba kama fursa ya kuongeza kasi ya ub...

Nderiananga: Kero za wananchi Sabasaba zisibaki kwenye makabrasha

Image
  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam. NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Ummy Nderiananga, amesisitiza kuwa kero na changamoto zinazowasilishwa na wananchi katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) zinapaswa kufuatiliwa hadi zipatiwe ufumbuzi, badala ya kuishia kupokelewa pekee. Nderiananga alitoa kauli hiyo alipotembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu, ambapo aliwataka wataalamu wanaotoa huduma kuhakikisha wanawasikiliza wananchi, wanarekodi kero zao na kuzifuatilia kwa karibu hadi hatua za utatuzi zikamilike. Aidha Aliupongeza uongozi wa banda hilo kwa maandalizi mazuri na kuisifu Idara ya Bunge na Siasa kwa kubuni mfumo unaowapa wananchi nafasi ya kuwasilisha changamoto zao moja kwa moja kwa Serikali na kupata mwongozo wa kuzitatua. "Ninawaelekeza wataalamu kuhakikisha kila kero inayowasilishwa hapa inafuatiliwa kwa ukaribu ili wananchi wapate majibu na suluhisho la changamoto zinazowakabili...

Serikali yatumia Sabasaba kusogeza huduma, kutatua kero za wananchi.

Image
  Na.Mwandishi wetu. WANANCHI wametakiwa kutumia Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) kutembelea banda la Ofisi ya Waziri Mkuu ili kupata huduma mbalimbali za Serikali, kuwasilisha kero zao na kupatiwa ufumbuzi pamoja na elimu kuhusu fursa za maendeleo. Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Profesa Palamagamba Kabudi, alipotembelea banda la Ofisi hiyo katika maonesho hayo, akisema Serikali imejipanga kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi kwa urahisi na kwa wakati. Alisema banda hilo limekusanya taasisi mbalimbali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), hatua inayowezesha wananchi kupata huduma nyingi katika eneo moja bila usumbufu. "Tunawakaribisha wananchi wote kufika katika banda letu kupata elimu, huduma mbalimbali za Serikali na kuwasilisha changamoto zao ili zipatiwe ufumbuzi kwa wakati,...

TTCL YAENDELEA KUWEKEZA KATIKA VITENDEA KAZI, YAKABIDHI MAGARI SITA

Image
  Na.Mwandishi wetu Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kutekeleza mkakati wake wa kuboresha mazingira ya kazi kwa kukabidhi magari sita (6) mapya yenye thamani ya Shilingi milioni 903 kwa Meneja wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Meneja wa Network Operations and Maintenance pamoja na Meneja wa Network Planning, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa shughuli za kiutendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi. Makabidhiano hayo yaliyofanyika leo katika Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam, ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL mnamo Aprili 29, 2026, wakati Shirika lilipokabidhi magari kwa baadhi ya viongozi wa idara mbalimbali, ambapo aliahidi kuendelea kuwekeza katika vitendea kazi ili kuongeza tija na ufanisi wa Shirika. Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi wa Ufundi wa TTCL, Mhandisi Cecil Francis, alisema ununuzi wa magari hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Miaka 10 wa Shirika unaolenga k...

TOSCI yafungua milango ya soko la kimataifa kupitia mbegu bora

Image
  Na.Mwandishi wetu Taasisi ya Udhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imesema Tanzania imejijengea uwezo wa kuzalisha mbegu bora zinazokubalika katika masoko ya kimataifa, hatua inayofungua fursa mpya kwa wakulima na wawekezaji kunufaika na biashara ya mbegu ndani na nje ya nchi. Akizungumza katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Mkurugenzi Mkuu wa TOSCI, Nyasebwa Chimagu, alisema mafanikio hayo yametokana na uwepo wa maabara ya taifa yenye ithibati ya kimataifa inayohakikisha mbegu zinazozalishwa nchini zinakidhi viwango vinavyotambulika duniani. Alisema uwezo huo unaenda sambamba na ajenda ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuimarisha kilimo biashara kupitia matumizi ya mbegu bora, ambazo ni msingi wa kuongeza uzalishaji na ushindani wa mazao katika soko la kimataifa. Chimagu alisema jukumu la TOSCI ni kusajili aina mpya za mbegu, wazalishaji pamoja na mashamba ya uzalishaji huku ikifanya ukaguzi katika kila hatua ili kuhakikisha mbegu zinazowa...

NACTVET YATUMIA SABASABA KUTOA HAMASA YA ELIMU YA AMALI, YAWAONESHA WANAFUNZI WENYE UJUZI WA VITENDO

Image
Na Mwandishi Wetu Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) linatumia Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) kutoa elimu kwa umma kuhusu majukumu yake ya kusimamia ubora wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, huku likitumia wanafunzi wa mkondo wa amali kuonesha matokeo ya maboresho ya mtaala wa elimu. Akizungumza na waandishi wa habari juni 2,2026 Afisa habari NACTVET, Dora Tesha, alisema maonesho hayo yamekuwa fursa muhimu ya kuwafikia wananchi, wazazi na wadau mbalimbali kwa kuwapa elimu kuhusu huduma zinazotolewa na baraza pamoja na nafasi ya elimu ya amali katika kuwaandaa vijana kujitegemea. Alisema jukumu kuu la NACTVET ni kusimamia utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi nchini ili kuhakikisha vyuo vinatoa mafunzo yenye viwango vinavyokubalika na yanayozalisha wahitimu wenye ujuzi unaohitajika katika soko la ajira. Tesha alisema katika banda la NACTVET wananchi wanapata huduma mbalimbali ikiwemo taar...