HALOTEL yaleta teknolojia za kisasa sabasaba,yasukuma mageuzi ya kidigital

 


Na Mwandishi Wetu


Kampuni ya mawasiliano ya Halotel Tanzania imezindua rasmi ushiriki wake katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), maarufu kama SabaSaba, kwa kuwasogezea wananchi huduma za kisasa za mawasiliano na kifedha zinazolenga kuharakisha mageuzi ya kidigitali nchini.

Ikiwa na kauli mbiu ya "Teknolojia kutoka Moyoni," Halotel imesema maonesho hayo ni fursa ya kuwaonesha wananchi na wadau suluhisho mbalimbali za kidigitali zinazorahisisha maisha ya kila siku na kusaidia ukuaji wa uchumi.

Pia,Wageni wanaotembelea banda la kampuni hiyo wanapata nafasi ya kujionea huduma za mtandao wa 5G, intaneti ya kasi ya juu ya HaloFibre, suluhisho za kidigitali kwa biashara pamoja na huduma za kifedha kupitia HaloPesa.

Akizungumza katika uzinduzi wa banda hilo leo Juni,2026 kwenye maonesho ya 50 ya kimataifa ya biashara,Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Halotel Tanzania, Bw. Abdallah Salum, alisema maonesho ya SabaSaba yanatoa nafasi ya kampuni hiyo kukutana ana kwa ana na wateja wake na kuwaonesha ubunifu unaoboresha maisha yao kupitia teknolojia.

Amesema Halotel itaendelea kuwekeza katika huduma zinazokidhi mahitaji ya wananchi huku ikihakikisha teknolojia inakuwa chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Tanzania, Bi. Tran Thi Thuy Dung, alisema kampuni hiyo imejipanga kuendelea kuwekeza katika suluhisho bunifu yanayoboresha uzoefu wa wateja na kuharakisha mageuzi ya kidigitali nchini.

Ameongeza kuwa kupitia maonesho hayo, wananchi wanapata fursa ya kujionea kwa vitendo namna huduma za Halotel zinavyorahisisha shughuli mbalimbali za kila siku.

Naye Meneja wa Masoko wa HaloPesa, Bi. Aidat Lwiza, amesema kuelekea maadhimisho ya miaka 10 ya huduma hiyo, kampuni imeandaa ofa maalumu, zawadi na shughuli mbalimbali zitakazowanufaisha wateja watakaotembelea banda la Halotel

Amesema kampeni hiyo inalenga kuongeza matumizi ya huduma za kifedha kidigitali na kuwafikia Watanzania wengi zaidi kwa huduma salama, rahisi na zenye uhakika.

Halotel imewaalika wananchi, wadau wa biashara na washiriki wote wa Maonesho ya 50 ya DITF kutembelea banda lake kuanzia Juni 28 hadi Julai 13, 2026, ili kujionea teknolojia mpya na kunufaika na ofa mbalimbali zilizoandaliwa kwa kipindi chote cha maonesho.

Comments

Popular posts from this blog

HAPI AWATAKA WAGOMBEA WALIOKOSA UTEUZI KUVUNJA MAKUNDI NA KUUNGANA KUTAFUTA KURA ZA KISHINDO ZA CHAMA HICHO.

Msajili Hazina aipa tano TPA

YUSUPH RAI AWASII WANANCHI TEMEKE KUCHAGUA MTU SIO CHAMA KWA MAENDELEO YA JIMBO HILO.