Nderiananga: Kero za wananchi Sabasaba zisibaki kwenye makabrasha

 


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.


NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Ummy Nderiananga, amesisitiza kuwa kero na changamoto zinazowasilishwa na wananchi katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) zinapaswa kufuatiliwa hadi zipatiwe ufumbuzi, badala ya kuishia kupokelewa pekee.

Nderiananga alitoa kauli hiyo alipotembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu, ambapo aliwataka wataalamu wanaotoa huduma kuhakikisha wanawasikiliza wananchi, wanarekodi kero zao na kuzifuatilia kwa karibu hadi hatua za utatuzi zikamilike.

Aidha Aliupongeza uongozi wa banda hilo kwa maandalizi mazuri na kuisifu Idara ya Bunge na Siasa kwa kubuni mfumo unaowapa wananchi nafasi ya kuwasilisha changamoto zao moja kwa moja kwa Serikali na kupata mwongozo wa kuzitatua.

"Ninawaelekeza wataalamu kuhakikisha kila kero inayowasilishwa hapa inafuatiliwa kwa ukaribu ili wananchi wapate majibu na suluhisho la changamoto zinazowakabili," alisema Nderiananga.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri pia alizungumza ana kwa ana na baadhi ya wananchi waliofika katika banda hilo, akisikiliza changamoto zao, kutoa ushauri wa kitaalamu na kuwaunganisha na wizara na taasisi husika kwa hatua zaidi za utatuzi.

Aidha, alitembelea idara na taasisi mbalimbali zilizopo ndani ya Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu, ikiwemo TACAIDS, ambapo alipata huduma ya kupima afya, huku akihimiza wananchi kutumia maonesho hayo kupata elimu na huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali.

Comments

Popular posts from this blog

HAPI AWATAKA WAGOMBEA WALIOKOSA UTEUZI KUVUNJA MAKUNDI NA KUUNGANA KUTAFUTA KURA ZA KISHINDO ZA CHAMA HICHO.

Msajili Hazina aipa tano TPA

YUSUPH RAI AWASII WANANCHI TEMEKE KUCHAGUA MTU SIO CHAMA KWA MAENDELEO YA JIMBO HILO.