Posts

FURAHA KWA WATEJA CRDB: WASHINDA SAFARI YA KOMBE LA DUNIA 2026, WENGINE WATINGA NA TV ZA KISASA INCHI 85.

Image
  Na Mwandishi Wetu Furaha na shangwe vimetawala kwa baadhi ya Watanzania baada ya kujikuta wakishinda zawadi nono kupitia kampeni ya “Tembo Card Visa” ya Benki ya CRDB, huku wanne wakipata nafasi ya kipekee ya kusafiri kwenda Marekani kushuhudia fainali za Kombe la Dunia 2026. Washindi hao, waliopatikana kupitia droo ya kwanza iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam, wameeleza hisia zao za mshangao na furaha, wakisema hawakutarajia kupata nafasi hiyo adhimu katika maisha yao. Miongoni mwa washindi wa safari hiyo ni Kenneth Masana Bina kutoka Kagera, Gasper Melkiory Kavishe wa Morogoro, pamoja na wakazi wa Dar es Salaam Arnold John Samugabo na Erick Harison Mlinga. Mbali na safari hiyo ya kihistoria, washindi wengine watatu walijishindia runinga janja (Smart TV) za inchi 85 pamoja na dishi na kifushi, wakisema zawadi hizo zitabadilisha namna wanavyofurahia burudani majumbani mwao. Akizungumza mara baada ya droo hiyo, Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Kadi wa CRDB, Karington Chahe, amese...

Njia Mpya za Usafirishaji Mirungi Zafichuliwa, Serikali Yaonya Kuongezeka kwa Mtandao wa Baharini.

Image
  Na Mwandishi wetu, Pwani MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imebaini kuibuka kwa njia mpya za usafirishaji wa dawa za kulevya kwa kutumia bahari, kufuatia kukamatwa kwa boti ya mwendokasi iliyokuwa ikisafirisha mirungi kutoka Mombasa, Kenya hadi Bagamoyo mkoani Pwani. Operesheni hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia Aprili 14, 2026 katika ufukwe wa Magambani, eneo la Kaole Ufundi, ilipelekea kukamatwa kwa viroba 18 vyenye paketi 1,062 za mirungi pamoja na watuhumiwa wanne wanaodaiwa kuhusika na mtandao huo. Akizungumza leo Aprili14,2026 Bagamoyo Pwani, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amesema tukio hilo linaonesha mabadiliko ya mbinu zinazotumiwa na wasafirishaji wa dawa za kulevya, ambapo sasa wanatumia njia za baharini kukwepa ulinzi uliopo nchi kavu. Alisema boti hiyo imekuwa ikifuatiliwa kwa muda mrefu, ikihusishwa na usafirishaji wa mirungi kutoka Mombasa kuja Dar es Salaam, hali inayothibitisha kuwepo kwa mtandao mpana unaoratibiwa kuvusha dawa...

MJUMBE WA JUMUIA YA MADOLA RAIS MSTAAFU CHAKWERA AKUTANA NA INEC

Image
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele leo Aprili 14, 2026 amekutana na kuzungumza na mjumbe maalum Jumuiya ya Madola (Commonwealth) Rais wa zamani wa Malawi Mhe.Lazarus McCarthy Chakwera ambaye alitembelea ofisi za Tume Njedengwa jijini Dodoma. Ziara hiyo maalum ya mjumbe huyo wa Jumuia ya Madola ililenga kuangalia namna Uchaguzi Mkuu wa 2025 ulivyofanyika. (Picha na INEC).

Mitandao mipya ya dawa za kulevya yaibuliwa; DCEA yaonya matumizi ya mbinu za kisasa usafirishaji

Image
  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imebaini kuibuka kwa mitandao mipya ya usafirishaji wa dawa za kulevya inayotumia mbinu za kisasa kuficha bidhaa hizo haramu, hali inayozua tahadhari mpya kwa vyombo vya usalama na wananchi. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo, amesema wahalifu wameanza kutumia njia zisizo za kawaida kusafirisha dawa hizo, ikiwemo kuzificha kwenye mizigo ya nguo za mitumba, matunda kama maembe, pamoja na ndani ya mifumo ya hewa (AC) ya mabasi. Amesema mabadiliko hayo ya mbinu yanakuja kufuatia kuimarishwa kwa udhibiti katika bandari na mipaka, jambo lililowalazimu wahusika wa biashara hiyo kubuni njia mbadala za kusafirisha dawa hizo ndani ya nchi. “Tunashuhudia wahalifu wakibadilika na kuja na mbinu mpya kila wakati, lakini sisi pia tunaendelea kuimarisha mikakati ya kukabiliana nao,” amesema Lyimo. Katika operesheni zilizofanyika mwezi Machi 2026, mamlaka hiyo ilifa...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO APRIL 13/2026

Image
 

Tanzania yang’ara Tuzo za Utalii Duniani, yaingiza vipengele 41.

Image
  Na.Mwandishi wetu.Dar es salaam TANZANIA imeendelea kung’ara katika anga la kimataifa baada ya kuingiza vipengele 41 katika Tuzo za Utalii na Usafirishaji Duniani (World Travel Awards), hatua inayoimarisha nafasi yake kama moja ya vinara wa utalii barani Afrika. Akizungumza, Aprili 11,2026 jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Paulina Mkama, amesema tuzo hizo zinahusisha jumla ya washindani 85 kutoka sekta za umma na binafsi, zikilenga kutambua na kusherehekea ubora wa huduma, kuhamasisha ushindani na kutoa fursa kwa wadau na watalii kupigia kura vivutio bora duniani. Paulina  ameeleza kuwa ushiriki wa Tanzania katika tuzo hizo ni fursa adhimu ya kuitangaza nchi kimataifa na kuiweka katika ramani ya dunia kama kitovu cha utalii.  Ameongeza kuwa taasisi za serikali, ikiwemo TFS na TAWA, zimefanikiwa kuwasilisha vivutio vyake katika kinyang’anyiro hicho. Kwenye kinyang’anyiro hicho , Tanzania imewania nafasi katika vipenge...

Watumishi Tume ya Uchaguzi watakiwa kuepuka uchochezi, wajipanga uchaguzi Isimani.

Image
  Na Mwandishi Wetu, Morogoro Watumishi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia katiba, sheria, kanuni  na taratibu na kuepuka lugha zozote za uchochezi zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani na kuhatarisha maisha ya Watanzania. Hayo yamesemwa leo Aprili 11, 2026 na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu), Dkt. James Henry Kilabuko kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt Jimmy Yonaz wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, katika kikao kilichoketi Mkoani Morogoro.  “Napenda kuwaasa, kuzingatia katiba, sheria, kanuni  na taratibu mnapotekeleza majukumu ya Tume na kuepuka lugha zozote za uchochezi zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani na kuhatarisha maisha ya Watanzania,”alisema Dkt Kilabuko.   Dkt. Kilabuko amesema, taasisi ina malengo yake, upo uwezakano wa kuepusha migogoro ya ndani na nje ya taasisi inayoweza kuathiri utekelezaji wa ma...