MNDEJEMBI AWAHAKIKISHIA WAKAZI WA KIGAMBONI UMEME WA UHAKIKA*
📌Afanya Ziara katika Kituo cha Dege 📌Aelekeza hatua za haraka kuchukuliwa kunusuru hali ya umeme Kigamboni 📌Umeme wa Megawati 22 kupatikana kwa hatua za haraka 📌Upanuzi wa Kituo cha Dege wafikia asilimia 60 Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi amefanya ziara ya kikazi ndani ya Mkoa wa kitanesco wa Kigamboni na kuagiza kuchukuliwa hatua za haraka za kuhakikisha hali ya umeme katika Mkoa wa Kigamboni inaboreshwa na kuwapa wakazi wa eneo hilo huduma ya uhakika alipotembelea Kituo cha Kupokea, Kupoza na Kusambaza umeme cha Dege tarehe 29 Novemba, 2025. “Leo tumekuja kuona ni namna gani Shirika letu la TANESCO linaweza kutatua changamoto hii kwa haraka zaidi na wameweka mipango mizuri ya muda mrefu katika kuhakikisha wanawezesha kupatikana kwa umeme wa uhakika kwa kujenga na kukiongezea nguvu Kituo cha Dege kwa kuweka transfoma ya MVA 120”, ameeleza Mhe. Ndejembi. Ili kukabiliana na changamoto ya huduma ya umeme iliyopo kwa haraka, Shirika limekuja na...