Posts

Showing posts from October, 2025

UCHAGUZI MKUU WA 2025 NI HALALI” – MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

Image
  Na Mwandishi wetu  Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza S. Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2025 unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba, 2025 ni halali kwakuwa umefuata misingi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria za Uchaguzi. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyasema hayo katika Mkutano na Vyombo vya Habari uliofanyika Ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma, tarehe 28 Oktoba, 2025. Akizungumza katika mkutano huo Mhe. Johari amesema kuwa Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameeleza kuwa, ni haki ya kila Mtanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.  “Ibara ya 5(1) ya Katiba yetu inatoa haki kwa kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane kupiga kura katika uchaguzi un...

WAPIGA KURA 37,647,235 KUPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29, 2025

Image
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na wananchi wakati akisoma risala yake kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotaraji kufanyika Oktoba 29, 2025.   

TANESCO YAANDIKA HISTORIA MPYA MIKOA YA LINDI NA MTWARA; YAWASHA MTAMBO WA KUZALISHA UMEME KWA GESI ASILIA WA MEGAWATI 20

Image
  *📌Uwezo wa uzalishaji umeme wapanda hadi megawati 77.5* 📌*RC Mtwara auzindua mradi na kupongeza Wizara ya Nishati na TANESCO kwa jmageuzi katika sekta ya nishati*  *📌Atoa Wito kwa Wawekezaji Kuchangamkia Fursa Mpya za Viwanda Mikoa ya Kusini* *📌sasa umeme unaozalishwa unakidhi mahitaji na kubaki na ziada*  Na Gloria Kalist Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeandika historia mpya Mikoa ya Lindi na Mtwara baada ya kuzindua rasmi mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia wenye uwezo wa megawati 20 katika Kituo cha Mtwara II, Uzinduzi huu ni hatua muhimu katika utekelezaji wa mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita wa kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu na endelevu nchini. Uwekezaji huu umeongeza uwezo wa kituo hicho kutoka megawati 57.5 hadi kufikia megawati 77.5 na hivyo kulifanya eneo la Kusini liwe na ziada ya umeme kwa mahitaji ya Viwanda, biashara na ajira mpya kwa wananchi kujiajiri katika biashara. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, ...

SERIKALI YAWATAKA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI NCHINI.

Image
Na Sophia Kingimali. Serikali imewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, ikisisitiza kuwa kupiga kura ni haki ya kikatiba huku kulinda amani ni wajibu wa kila Mtanzania. Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, ,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo, alitoa wito huo katika Kongamano la Kitaifa la Amani lililofanyika Leo Octoba 27,2025 jijini Dar es Salaam, likiwa na kaulimbiu “Kupiga kura ni haki yetu, kuilinda amani ni wajibu wetu.” Prof. Mkumbo amewahimiza Watanzania kutumia uchaguzi kama jukwaa la kuimarisha maendeleo na utulivu wa taifa.  “Maendeleo ni mchakato endelevu. Tutumie uchaguzi huu kuwachagua viongozi watakaotupeleka mbele katika dira ya amani na maendeleo tunayoitamani,” amesema. Prof. Mkumbo ameishukuru Kamati ya Amani ya Kitaifa kwa kuandaa makongamano hayo nchini kote, kwani  yamerudish...

KINYOGOLI AWATAKA WANANCHI MBAGALA KUCHAGUA MAENDELEO.

Image
  Na Sophia Kingimali. MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Mbagala kupitia Chama cha Wananchi (CUF),Sheik Said Kinyogoli, ameahidi kupigania maslahi ya wananchi wa jimbo hilo endapo atachaguliwa kuwa Mbunge katika uchaguzi mkuu ujao, akisisitiza kuwa muda wa maneno umeisha na sasa ni wakati wa matendo. Akizungumza wakati wa kufunga kampeni zake za ubunge katika jimbon hilo zilizofanyika jana katika eneo la Mbagala Kijichi, Kinyogoli amesema wananchi wa jimbo hilo wanahitaji kiongozi atakayesimama kuwasemea bungeni na sio wabunge wanaokaa kimya bila kuchangia hoja muhimu. “Jimbo letu lazima lipate mtu wa kulipigia kelele ili tupone. Tunaambiwa elimu bure, lakini wazazi bado wanachangia hadi mishahara ya walimu. Mwaka huu hatucheki na yeyote, tunataka ushindi ili tuiseme Mbagala yetu,” alisema Kinyogoli huku akishangiliwa na umati wa wananchi. Aidha, Kinyogoli amewataka wananchi kuachana na ushabiki wa vyama na badala yake kumchagua kiongozi mwenye uwezo wa kuwatumikia kwa vitendo. “Sasa hivi...

Viongozi wa dini Kanda ya Kati wataka amani uchaguzi mkuu

Image
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma VIONGOZI wa dini mbalimbali kutoka Kanda ya Kati  wamewataka Watanzania kuendelea kulinda amani ya nchi na kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025, wakisisitiza kuwa amani ni tunu na urithi wa thamani unaopaswa kulindwa na kila raia. Wito huo umetolewa leo Oktoba 25, 2025, katika Kongamano la Amani lililofanyika jijini Dodoma, likijumuisha viongozi wa dini kutoka mikoa ya Dodoma na Singida. Katika kongamano hilo, viongozi hao walijadili mada mbalimbali kuhusu umuhimu wa kupiga kura, historia ya chaguzi nchini na wajibu wa kila raia kulingana na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Akitoa mada kuhusu umuhimu wa amani, Mwenyekiti wa Baraza la Makanisa ya Kikristo Tanzania (CCT) Mkoa wa Dodoma na Askofu wa Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT), Joseph Mtolela, amesema Tanzania imeendelea kuwa kisiwa cha amani katika kipindi chote cha kampeni, na hivyo ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha hali hiyo in...

Mradi wa TACTIC utanufaisha wananchi wa Mpanda- Mrindoko

Image
  Na Mwandishi wetu Katavi MKUU wa Mkoa wa Katavi, Mhe.Mwanamvua Mrindoko, amesema utekelezaji wa Mradi wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) katika Mji wa Mpanda utaleta mabadiliko chanya kwa wananchi na wageni katika utoaji huduma na mahitaji mbalimbali ya usafiri na usafirishaji, mazingira bora ya shughuli za kiuchumi na ongezeko la mapato kwa Halmashauri. Mhe. Mrindoko aimeitaka Halmashauri ya Manispaa kufanya tathmini ya miradi yenye kujiendesha ihakikishe inaboresha huduma kuwa rafiki zaidi kwa wote pamoja na kuongeza mapato kwa Halmashauri na Serikali kwa ujumla. Rai hiyo ameitoa leo Oktoba 25, 2025, wakati wa hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa miundombinu kupitia Mradi wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC), wenye thamani ya Sh. bilioni 21.9, ambao utajumuisha ujenzi wa barabara 10 kwa kiwango cha lami, ujenzi wa jengo la usimamizi wa mradi na ununuzi magari manne ya kusimamia utekelezaji wa mradi. "Natoa rai kwa Mkandarasi kuhakikisha...