Wanafunzi wanaokwenda kusoma nje ya nchi wafundwa.
Na. Sophia Kingimali Wito umetolewa kwa wanafunzi wanaokwenda kusoma nje ya nchi kutumia fursa wanazopewa kwa nidhamu, bidii na kuzingatia maadili, ili wakirejee walete mchango chanya kwa maendeleo ya Taifa. Wito huo umetolewa leo Januari 30,2026 katika hafla ya kuwaaga wanafunzi 16 kati ya 50 wa programu ya Samia Scholarship Extended DS/AI, iliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, amewasisitiza wanafunzi hao kuwa mabalozi wa nchi na kuhakikisha wanajifunza kwa bidii, wanaheshimu sheria za nchi wanazoenda "Mkatumie maarifa mtakayopata kuleta suluhisho la changamoto za maendeleo hapa nchini ili kupata mabadiliko chanya kulingana na dira ya maendeleo ya 2050",Amesema Prof. Mkenda. Profesa Mkenda amesema programu ya Samia Scholarship ni matokeo ya dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuwekeza kwenye sayansi, teknolojia na rasilimali watu, hususan kwa vijan...