MHANDISI MATIVILA AKAGUA MIRADI YA DMDP II, ATOA WITO UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU
πTARURA kujenga takribani Km. 250 za barabara Manispaa zote za Dar es Salaam Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila, amesema Serikali kupitia TARURA inaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu mkoa wa Dar es Salaam Awamu ya Pili (DMDP II) huku akiwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika utunzaji wake ili idumu kwa muda mrefu. Ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi wa DMDP II katika Manispaa za Ubungo na Kinondoni, akisisitiza umuhimu wa kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati ili kuboresha miundombinu na maisha ya wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam. Mhandisi Mativila alikagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara ya Msumi Km 9.9 na daraja la Msumi na ujenzi wa barabara ya Goba Wakorea km 7.76 zilizopo Ubungo pamoja na ujenzi wa barabara ya Mivumoni Km 4.79 iliyopo Kinondoni ambapo uteke...