Taasisi za Umma zatakiwa kutokuwa kikwazo kwa wawekezaji
Na Mwandishi wa OTR Pwani. Serikali imezitaka Taasisi za Umma kuhakikisha zinakuwa chachu ya ukuaji wa uchumi kwa kutengeneza mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji kupitia mifumo yenye ufanisi, kupunguza urasimu usio wa lazima, kuboresha utoaji wa huduma na kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi katika kuunga mkono utekelezaji wa Dira 2050. Wito huo ulitolewa Julai 24,2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, wakati akifunga awamu ya tatu ya Programu ya Mafunzo Elekezi ya siku nne kwa Watendaji Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha mkoani Pwani. Akizungumza na viongozi hao, Mhe. Kikwete alisema mafanikio ya Dira 2050 hayatategemea ubora wa sera na mipango pekee, bali namna taasisi za umma zitakavyotekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuzalisha matokeo yanayoonekana kwa wananchi na kwa uchumi wa Taifa. Amewataka Wakuu wa Taasisi za Umma ku...