TANESCO YAKUTANA NA WADAU MOROGORO KUJADILI MIKAKATI YA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI BWAWA LA JNHPP.
📌 Ni kufuatia utafiti uliofanywa na TANESCO kutambua vihatarishi na hatua za kuchukua kunusuru vyanzo Vya mito. 📌RC Malima aongoza kikao hicho na kukubaliana hatua za kudhibiti mapema Morogoro Septemba 26,2025. Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limekutana na wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali, Uongozi wa Mkoa wa Morogoro, pamoja na wataalamu wa mazingira, maji na nishati, katika kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, kwa lengo la kujadili vihatarishi na mikakati ya kulinda vyanzo vya maji vinavyopeleka maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme, hususani Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere. Kikao hicho kimeongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima, na kuhudhuriwa na wakuu wa wilaya za Morogoro, Ulanga, Malinyi na Ifakara, pamoja na viongozi waandamizi wa TANESCO wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Bwana Lazaro Twange. Katika kikao hicho, wadau wamejadili kwa kina vihatarishi vinavyojitokeza sasa na ambavyo visipodhibitiwa mape...