Posts

Showing posts from February, 2026

SERIKALI YADHAMIRIA KUMALIZA CHANGAMOTO YA USAFIRI DAR ES SALAAM

Image
  NA. MWANDISHI WETU – Dar es Salaam KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Dkt. Jim Yonazi ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa DART amesema Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha inamaliza changamoto ya usafiri katika Jiji la Dar es Salaam, ili wananchi waweze kupata huduma bora, ya haraka na yenye uhakika. Akizungumza hii leo 27 Februari, 2026 mara baada ya Kamati hiyo kufanya ziara ya kukagua miundombinu ya usafirishaji jijini humo, Dkt. Yonazi amesema Serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa katika kuboresha sekta ya usafiri wa umma. Alisema katika ziara hiyo, kamati ilitembelea Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) pamoja na Kampuni ya Uendeshaji wa Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) na kujionea maendeleo ya uwekezaji uliofanywa. “Ni dhamira ya Serikali kuhakikisha usafiri wa Dar es Salaam unakuwa bora, wa kisasa na unaokidhi mahitaji ya wananchi. Tumejionea miundombinu iliyowekwa na jitihada zinazoendelea...

BRELA YAWAKUMBUSHA WAJASIRIAMALI NCHINI KURASIMISHA BIASHARA ZAO.

Image
 Na.Mwandishi wetu. Wakala wa Usajili wa Biashara la Leseni (BRELA) imewataka wajasiriamali wa bidhaa mbalimbali za viwanda kurasimisha biashara zao ili kuendelea kunufaika na fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana nchini na nje ya nchi. Wito huo umetolewa leo tarehe 27 Februari ,2026 na Msaidizi wa Usajili Mkuu kutoka BRELA Bi. Hellen Mhina wakati akizungumzia ushiriki wa Wakala kwenye Maonyesho ya sita (6) ya Bidhaa za Viwanda na Biashara za Wanawake Tanzania yanayofanyika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika maonyesho hayo, Bi. Mhina alisema BRELA imesogeza huduma za papo kwa papo katika viwanja hivyo kwa lengo la kuwasaidia wajasiriamali wa biadhaa za viwanda pamoja na wananchi kwa ujumla wake kuzifikia huduma za BRELA.  “Tunashiriki maonyesho haya kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi na wafanyabiashara wenye changamoto za kimfumo ili waweze kutatuliwa changamoto zao, tunatoa pia elimu juu ya Umiliki Manufaa kwa wamiliki wa kampuni l...

MAAFISA 659 TCTA WAJENGEWA UWEZO KUHUSU URASIMISHAJI WA BIASHARA

Image
  Na.Mwandishi wetu. Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeendelea kuimarisha juhudi za kuhamasisha urasimishaji wa biashara kwa kutoa mafunzo maalum kwa wanafunzi Maafisa wa Magereza wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), ikiwa ni sehemu ya kuwajengea uwezo wa kiuchumi mapema wakiwa bado kazini. Mafunzo hayo yalifunguliwa rasmi na Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa, ambaye alieleza kuwa lengo kuu ni kuwajengea maafisa hao uelewa wa kina kuhusu umuhimu wa kuanzisha na kurasimisha biashara zao kwa mujibu wa sheria. Alisisitiza kuwa urasimishaji wa biashara si tu unaleta uhalali wa kisheria, bali pia unafungua milango ya fursa mbalimbali za kifedha ikiwemo kupata tender mbalimbali. “Ni muhimu kwa watumishi kuanza mapema kuwekeza na kurasimisha shughuli zako kabla ya kustaafu, ili kujenga msingi imara wa maisha ya baadaye,” alisisitiza Bw. Nyaisa. Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha TCTA, SACP. Willingtone Kahumuza, alisema mafunzo hayo yanaendan...

KAMATI YA UONGOZI WA MRADI WA JNHPP YAKAGUA MAENDELEO YA BWAWA LA JULIUS NYERERE

Image
  📌Yasema mradi umesimamiwa na kutekelezwa kwa ufanisi 📌Yasisitiza ni kichocheo muhimu katika  fursa za kiuchumi na kijamii Kamati ya Uongozi wa Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP), tarehe 26 Februari 2026, imekagua maendeleo ya uzalishaji wa umeme katika bwawa la Julius Nyerere na kueleza kuridhishwa na usimamizi pamoja na utekelezaji wake, uliokidhi viwango vya ubora vinavyoendana na thamani ya fedha iliyowekezwa na Serikali. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Dkt. Jim Yonazi , amesema kamati imefurahishwa na namna bwawa hilo linavyochochea ukuaji wa uchumi kwa kuongeza uzalishaji wa umeme unaosambazwa katika maeneo mbalimbali nchini, hatua inayochangia kuimarika kwa upatikanaji wa nishati ya umeme. “Tumeridhishwa na jinsi mradi huu ulivyosimamiwa na kutekelezwa kwa ufanisi mkubwa. Ukilinganisha na miradi mingine barani Afrika, mradi huu umejengwa kwa ubora wa hali ya juu na umeleta unafu...

MIF 2026 kujadili mikakati ya kufikia uchumi wa kati wa juu 2050

Image
  Dar es Salaam.  Serikali imesema Mkutano wa Jukwaa la Wakurugenzi wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Kampuni ambazo Serikali ina hisa chache (Minority Interests Forum-MIF 2026) utakuwa jukwaa mahususi la kujadili, pamoja na mambo mengine, mikakati ya kuharakisha safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati wa juu ifikapo mwaka 2050. Mkutano huo, unaoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH), utafanyika kuanzia Machi 16 hadi 18, 2026 katika Ukumbi wa PAPU, jijini Arusha, na unatarajiwa kuwakutanisha Wakurugenzi wa Bodi na Watendaji Wakuu kati ya 150 na 200 kutoka kampuni 56 ambazo Serikali inamiliki hisa chache, yaani chini ya asilimia 51. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam Februari 24, 2026, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Utendaji, Ufuatiliaji na Tathmini – Mashirika ya Kibiashara, Bi. Lightness Mauki, alisema kuwa safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati wa juu si ya kubahatisha, bali ni matokeo ya maamuzi ya kimkakati, usimamizi th...

WANANCHI PERAMIHO, SHIWINGA KUPIGA KURA KESHO KUCHAGUA MBUNGE, DIWANI

Image
 Na Mwandishi wetu, Ruvuma Wapiga Kura 127,632 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura watashiriki katika uchaguzi wa kuchagua Mbunge katika Jimbo la Peramiho lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma na Kata ya Shiwinga iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe.   Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele ameyasema hayo leo Februari 25, 2026 mjini Songea Mkoani Ruvuma wakati akisoma risala maalum kuhusu uchaguzi katika jimbo na kata husika utakao fanyika kesho Februari 26, 2026 na kusema kuwa jumla ya vituo 373 vya Kupigia Kura vitatumika.   “Kati yao wapiga kura 120,780 ni wa Jimbo la Peramiho na wapiga kura 6,852 wapo katika kata ya shiwinga na jumla ya vituo 373 vya Kupigia Kura vitatumika, ambapo vituo 354 vipo Jimbo la Peramiho na vituo 19 vipo katika Kata ya Shiwinga Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi,”amesema Jaji Mwambegele.   Aidha, amesema kwa uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la ...

INEC YAWAFUNDA WASIMAMIZI NA WASIMAMIZI WA SAIDIZI WA VITUO VYA KURA JIMBO LA PERAMIHO

Image
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele leo Februari 23, 2026 ametembelea mafunzo ya Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya vituo katika Jimbo la Peramiho lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma na kuzungumza nao ambapo amewasisitiza kutekeleza majukumu yao kwa weledi kwa kufuata Sheria, Kanuni na maelekezo ya Tume. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele leo Februari 23, 2026 ametembelea mafunzo ya Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya vituo katika Jimbo la Peramiho lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma na kuzungumza nao ambapo amewasisitiza kutekeleza majukumu yao kwa weledi kwa kufuata Sheria, Kanuni na maelekezo ya Tume. Mafunzo hayo ya siku mbili yalifanyika katika Kumbi tatu tofauti za  Seminari Kuu Peramiho, Maposeni Sekondari na Ukumbi wa Josephat Mkuwa  ni maandalizi ya Uchaguzi Mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Peramiho ambao un...

Mapinduzi makubwa yafanyika sekta ya madini wachimbaji wadogo kuwezeshwa mitaji.

Image
  Na.Mwandishi wetu. ☑️ Waziri Mavunde Asisitiza Hatua Hiyo ni Utekelezaji wa Maelekezo ya Mhe. Rais Dkt Samia  ☑️ Makubaliano Maalum ya Kihistoria Yafungua Milango ya Mitaji, Teknolojia na Ukuaji wa Wachimbaji Wadogo  ☑️ Kikundi cha Songwe Gold Family Kupokea Mkopo wa Tsh Bilioni 50 kwa Mkupuo na Kuvunja Rekodi kwa Wachimbaji Wadogo 📍 Dar es Salaam  Katika hatua ya kihistoria na mageuzi ya Sekta ya Madini nchini, Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini leo Februari 23, 2026 imesaini Makubaliano Maalum na Benki ya CRDB yatakayorahisisha upatikanaji wa huduma za fedha kwa wachimbaji wadogo wa madini.  Akizungumza katika hafla hiyo ya kihistoria iliyofanyika katika jijini Dar es Salaam, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa utashi na uongozi thabiti unaoendelea kuibadilisha Sekta ya Madini kuendelea kuwavutia wawekezaji . Waziri Mavunde amesisitiza kuwa hatua hiyo ni...

BRELA Yaimarisha Usalama Kazini kwa Mafunzo ya Kukabiliana na Majanga ya Moto

Image
  Na.Mwandishi wetu. Watumishi wa Wakala wa Usajili wa Leseni na Leseni  (BRELA) wamepatiwa mafunzo maalum ya kukabiliana na majanga ya moto mahali pa kazi, yaliyotolewa na maafisa kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, kwa lengo la kuongeza usalama na utayari wa watumishi dhidi ya majanga ya moto. Mafunzo hayo yaliyofanyika (jana) tarehe 20 Februari 2026 katika Ofisi za BRELA yalilenga kuwawezesha watumishi kutambua aina za moto, kutumia kwa usahihi vifaa vya kuzimia moto pamoja na kuchukua hatua stahiki pindi majanga yanapotokea ndani au nje ya majengo ya kazi. Akizungumza baada ya mafumzo hayo, Afisa wa BRELA Bw. John Machela alisema mafunzo hayo yameongeza uelewa na uwezo wa vitendo katika kukabiliana na majanga ya moto siyo tu kazini bali hata majumbani. “Mafunzo haya yametusaidia kujiandaa kikamilifu pindi changamoto za majanga ya moto zinapotokea. Yamenisaidia binafsi hata nikiwa nyumbani, kwani sasa ninaelewa namna sahihi ya kujilinda na kujiokoa,” alisema Bw. Machela. A...

NSSF YAIBUKA MSHINDI, YATUNUKIWA TUZO KWA TAASISI ZILIZOFANYA VIZURI KATIKA KUZINGATIA SHERIA.

Image
Na.Mwandishi wetu Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umeibuka mshindi wa kwanza na kutunukiwa tuzo kwa  Taasisi zilizofanya vizuri katika uzingatiaji wa Sheria ya Serikali Mtandao, viwango na miongozo kwa taasisi zilizo katika ngazi ya nne ya ukomavu wa TEHAMA Serikalini.

MAKAMU MWENYEKITI INEC NA WAJUMBE WA TUME WAMTEMBELEA RC SONGWE

Image
Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk leo Februari 19, 2026 akiwa na Mjumbe wa Tume, Mhe. Dkt. Zakia Mohamed Abubakar wamemtembelea  ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Jabiri Omari Makame.  Viongozi hao wa Tume wapo mkoani humo kwa ziara ya kikazi ambapo wametembelea na kukagua maandalizi ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Shiwinga, Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, Mkoani Songwe unaotarajiwa kufanyika Februari 26, 2026.