Posts

Showing posts from April, 2026

PBPA YAHAMASISHA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Image
Na.Mwandishi wetu. Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) umechukua hatua madhubuti ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwa kuwagawia watumishi wake majiko ya umeme, ikiwa ni sehemu ya juhudi za makusudi za kuhamasisha mabadiliko ya matumizi ya nishati nchini. Akizungumza katika tukio hilo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PBPA, Mhandisi Bruno Tarimo, amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha juhudi za taasisi katika kuelimisha jamii kuhusu matumizi ya nishati safi na salama kwa matumizi ya kila siku. Ameeleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia sera mbalimbali za kitaifa na kimataifa, imeendelea kutambua umuhimu wa nishati safi ya kupikia kama nyenzo muhimu ya kukabiliana na changamoto za kimazingira, kiafya, kijamii na kiuchumi. “PBPA inatekeleza jukumu muhimu katika kusaidia juhudi za Serikali za kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034. Ugawaji wa majiko janja aina ya pressure cooker kwa watumishi ni sehemu ya ...

DCEA NA TFS WASHIRIKIANA KUOANYA OPERESHENI KATIKA HIFADHI YA MSITU WA IGOMBE RIVER

Image
  Na.Mwandishi wetu. Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) pamoja na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Tabora, imefanya operesheni maalum katika hifadhi ya msitu wa Igombe river iliyopo wilaya ya Uyui na katika hifadhi ya msitu wa Nyahua iliyopo wilaya ya Skonge mkoani Tabora na kufanikiwa kuteketeza ekari 68 za mashamba ya bangi, kukamata gunia 133 za bangi huku watu saba (7) wakikamatwa katika operesheni hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 30 Aprili, 2026 katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Tabora, Kamishna Jenerali Aretas Lyimo amesema, Mamlaka iko kwenye operesheni maalum ya kuteketeza dawa za kulevya zinazozalishwa nchini.  “Sasa hivi tuko kwenye kampeni maalum kuhakikisha kwamba tunateketeza dawa za kulevya zinazozalishwa nchini baada ya dawa za viwandani kupungua” amesema Lyimo. Aidha, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha M...

WATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUSIMAMIA UCHAGUZI KWA WELEDI

Image
  Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakjati akifunga mafunzo ya watendaji wa uchaguzi yaliyofanyika Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo yamefungwa leo tarehe 30 Aprili, 2026 na yaliyofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 28 Aprili, 2026. Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakjati akifunga mafunzo ya watendaji wa uchaguzi yaliyofanyika Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo yamefungwa leo tarehe 30 Aprili, 2026 na yaliyofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 28 Aprili, 2026. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa rufani Jacobs Mwambegele akiwa katika ufungaji wa mafunzo hayo.  Na. Mwandishi Wetu, Morogoro Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetoa wito kwa watendaji wa uchaguzi kuhakikisha wanatumia muda wao kusoma Katiba, sheria za uchaguzi, kanuni na maelekezo ya Tume ili waweze kusimamia uchaguzi kwa w...

WATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUEPUKA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA

Image
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akizungumza Mkoani Morogoro leo tarehe 28 Aprili, 2026 wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa  watendaji wa uchaguzi. Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kisheria wa Tume, Ndg. Cyprian Mbugano akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Watendaji wa Uchaguzi na mambo muhimu ya kuzingatia.  Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Isimani na Kata 12 za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi. Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Isimani na Kata 12 za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi. Mkurugenziu wa Ofisi ya Zanzibar, Ndg. Adam Mkina akiwasilisha mada  Meza Kuu ikiwa katika ukumbi wa mafunzo Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Isimani na Kata 12 za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi. Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa, Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasai...

KAFULILA: MUUNGANO WA TANZANIA NI MUUNGANO WA WATU ZAIDI KULIKO SERIKALI NA SHERIA.

Image
  Hiki ndicho  alichoandika Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini PPPC Bwana David Kafulila kwenye Ukura wake wa X, amekumbusha kuwa, "Kwa kipindi cha miaka 62 mfululizo, Tanzania imekuwa mfano wa kipekee barani Afrika huu ndio muungano pekee wa mataifa mawili huru uliodumu kwa zaidi ya nusu karne.  Wakati miungano mingine kama Ethiopia–Eritrea (1952–1962), Ghana–Guinea–Mali (1958–1963), na Senegambia (1982–1989) ilivunjika mapema,  Tanzania imeendelea kusimama imara na kuonyesha mshikamano wa kipekee Duniani. Siri ya mafanikio haya haipo tu kwenye makubaliano ya kiserikali na kisheria bali kwenye asili ya udugu wa damu, mshikamano wa kijamii, na lugha ya Kiswahili inayotufanya tuwe taifa moja.  Huu ni muungano wa watu, uliojengwa juu ya historia ya pamoja na misingi thabiti ya mshikamano wa kitamaduni. Leo tunaposherehekea miaka 62 ya Muungano, tunawakumbuka kwa heshima kuu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume, waanzilishi wa saf...

DCEA yapokea vifaa vya kisasa vya uchunguzi kutoka UNODC.

Image
Na.Mwandishi wetu. Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imepokea vifaa vya kisasa vya uchunguzi wa kimaabara kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), ikiwa ni pongezi baada ya kutambua mafanikio yaliyofikiwa na Tanzania katika udhibiti wa dawa za kulevya nchini. Akikabidhi vifaa hivyo tarehe 22 Aprili 2026 jijini Dar es Salaam, Mwakilishi wa UNODC Kanda ya Afrika Mashariki, Ali El-Bereir, aliipongeza Tanzania kwa jitihada zake katika kudhibiti biashara na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na kemikali bashirifu. Vifaa hivyo vimetolewa mahsusi kuzijengea uwezo taasisi zinazoshughulikia udhibiti wa dawa za kulevya kimataifa kupitia mpango wa Port Security and Safety of Navigation Programme (EU PSP). Miongoni mwa vifaa hivyo ni mashine za kisasa zenye uwezo wa kubaini kwa haraka aina mbalimbali za dawa za kulevya na kemikali zinazodhibitiwa, hata zikiwa ndani ya vifungashio vyake bila kufunguliwa, hatua itakayoongeza ufan...

POSTA NA BODI YA MIKOPO ZASAINI USHIRIKIANO KURAHISISHA HUDUMA KWA VIJANA

Image
Na Sophia Kingimali Dar es Salaam.  Taasisi ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) imeingia makubaliano ya ushirikiano na Shirika la Posta Tanzania, hatua inayolenga kurahisisha huduma za maombi ya mikopo kwa vijana nchini. Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo,leo Aprili 22,2026 Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo,(HESLB) Dk. Bill Kiwia, amesema, ushirikiano huo na Posta utasaidia kutoa suluhisho kwa changamoto mbalimbali walizokuwa wakipata wanafunzi pindi wanapoomba mikopo hiyo. Amesema ofisi hizo zitatumika kusaidia vijana kujaza na kuwasilisha maombi ya mikopo, kufanya uhakiki wa nyaraka na kutoa msaada wa kitaalamu ili kuhakikisha wanakidhi vigezo vinavyohitajika. “Lengo letu ni kuhakikisha hakuna kijana anayekosa mkopo kwa sababu ya changamoto za kiufundi au kukosa msaada wa kujaza maombi,” alisisitiza Dk. Kiwia. Amesema tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo, zaidi ya trilioni tisa zimetolewa kama mikopo kwa wanufaika zaidi ya milioni moja, wakiwemo w...

WAZIRI NDEJEMBI AWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI 2026/27 BUNGENI

Image
  📌Asema kipaumbele ni kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini 📌 Uwezo wa uzalishaji umeme waongezeka kwa asilimia 12.17 📌Aeleza ongezeko hilo limechangiwa na kukamilika kwa miradi mbalimbali ya umeme Na.Mwandishi wetu. Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amewasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Bajeti  ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2026/2027, akiainisha vipaumbele  katika sekta ndogo ya umeme kuwa ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Akisoma hotuba ya bajeti hiyo Aprili 22, 2026, Bungeni Dodoma, Waziri Ndejembi ametaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na kuendeleza uzalishaji wa umeme kupitia mitambo tisa katika Kituo cha Kufua Umeme cha Bwawa la Julius Nyerere, kukamilisha awamu zinazofuata katika mradi wa kuzalisha umeme kwa nguvu ya jua Kishapu baada ya megawati 50 kuunganishwa kwenye gridi ya taifa na utekelezaji wa mradi wa umeme wa Malagarasi, Kigoma...

"NGUVU KAZI SHINDANI NI KETE YA DIRA 2050"- DAVID KAFULILA.

Image
  Na.Mwandishi wetu. Aeleza Jinsi PPP Ilivyo muhimu kwenye Uwekezaji wa Elimu na Afya. Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP-CENTRE), David Kafulila, amesema makusanyo ya kodi na mikopo pekee hayawezi kutosheleza mahitaji makubwa ya kuleta ustawi kwa Watanzania, hivyo ushirikishwaji wa sekta binafsi ni wa lazima. Kafulila amefafanua kuwa Serikali inayolazimisha kufanya kila kitu peke yake hujikuta ikishindwa kutoa huduma bora za msingi, hususani katika sekta za elimu na afya, ambazo ndio nguzo za kujenga rasilimali watu. Kafulila alihitimisha kwa kutoa dira ya kimkakati inayosukuma ajenda ya PPP. Alieleza kuwa iwapo Serikali itatumia mitaji ya sekta binafsi kujenga miundombinu, itaokoa fedha nyingi ambazo sasa zitapelekwa moja kwa moja kugharamia afya na elimu bora kwa jamii maskini isiyoweza kumudu gharama hizo. "Dunia ya leo tunazungumzia ushindani wa watu, sio vitu. Ushindani wa watu wenye ubora. Hawa watu wenye ubora unawatengeneza j...

KATIBU MKUU MATARAGIO AIPONGEZA PBPA KWA KUHAKIKISHA UWEPO WA MAFUTA YA KUTOSHA NCHINI

Image
Na.Mwandishi wetu. Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati (anayeshughulikia mafuta na gesi),Dkt. James Mataragio ameipongeza Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) kwa kuhakikisha nchi inakuwa na mafuta ya kutosha wakati wote. Ameyasema hayo leo Aprili 21,2026 alipotembelea Banda la PBPA katika Maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.  Akifafanua wakati wa ziara hiyo, Meneja wa Sheria, Bi. Lilian Rwegimbura amesema mpaka sasa mafuta yapo ya kutosha na ambayo yapo melini ni metriki tani lita milioni 42 hivyo PBPA inaendelea kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa mafuta.