MASANJA ATANGAZWA RASMI KUWA BALOZI WA MWANGAZA,AIOMBA SERIKALI KUSAPOTI WAWEKEZAJI WA NDANI.
Mtumishi wa Mungu, mtangazaji na msanii maarufu nchini, Emmanuel Mgaya(Masanja Mkandamizaji) ametangazwa rasmi kuwa balozi wa kampuni ya Kitanzania ya Mwangaza Stationery & Supply kwa lengo la kuwaelimisha Watanzania kuhusu matumizi ya vifaa bora na vya kisasa vya maofisini.
Pia,ametoa rai kwa serikali na taasisi zake zote nchini pamoja taasisi binafsi kuhakikisha wanaagiza vitendea kazi vya ofisini kwao kutoka kwa Mwangaza kwani hufanya hivyo ni kuendelea kutoa fursa za ajira kwa vijana lakini kusapoti uwekezaji wa ndani
Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo Septemba 24,2025 jijijini Dar es salaam Masanja amesema ameamua kushirikiana na Mwangaza kutokana na ubora wa bidhaa zao na huduma makini wanazotoa kupitia vijana wenye weledi.
"Kiukweli, kupitia Mwangaza, kile kilio cha watu wanaohitaji vifaa vya ofisini vyenye ubora wa hali ya juu kitapatiwa suluhisho. Vifaa vyao vina viwango vya kimataifa na vinapatikana kwa bei nafuu," alisema Masanja.
Aidha, aliwahimiza wafanyabiashara wa vifaa vya ofisini, taasisi za elimu, makampuni binafsi pamoja na wananchi kwa ujumla, kutumia bidhaa kutoka Mwangaza Stationery & Supply akisisitiza kuwa ni za kiwango cha juu na zinazokidhi mahitaji ya kisasa ya kiteknolojia na ufanisi kazini.
"Mwangaza si tu jina la kampuni, bali ni mwanga halisi kwa wale wanaotafuta bidhaa bora, huduma ya haraka, na gharama rafiki," aliongeza Masanja
Kampuni ya Mwangaza Stationery & Supply imejikita katika kutengeneza na kusambaza vifaa vya maofisini na skuli, ikiwa ni pamoja na karatasi, kalamu, mashine za ofisini na bidhaa nyingine za kipekee zinazowasaidia wafanyakazi kuongeza ufanisi katika mazingira ya kazi.
Kwa upande wao, uongozi wa kampuni hiyo umesema wanafurahishwa na ushirikiano huo na wana imani kuwa kupitia Masanja, Watanzania wengi zaidi wataweza kufahamu na kufikia bidhaa zao kwa urahisi zaidi.






Comments
Post a Comment