CHAMA CHA MAKINI WAMPA TANO DKT SAMIA KUTOKANA NA UONGOZI WAKE.

 


Na Sophia Kingimali.


Mgombea Urais kupitia Chama makini Coster Kibonde amesema pindi atakapopata ridhaa ya kuwa Rais atampa uongozi wa juu mgombea urais na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kutokana na umahiri wake wa uongozi.


Hayo ameyasema leo Septemba 2,2025 Jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho amesema Dkt Samia ni mwanadiplomasia mzuri kwani katika kipindi chake amefanya mambo mengi mazuri na hayapaswi kubezwa.


"Pindi wananchi watakaponipa ridhaa na tume huru kunitangaza kuwa Rais wa nchi hii viongozi wote walioingia kwenye mchakato wa kugombea nafasi ya urais nitawapa nafasi kwenye serikali yangu lakini nafasi ya kwanza nitampa Dkt Samia Suluhu Hassan kwani huyu ni mwana diplomasia mzuri na ninaamini atakwenda kuifanya kazi nzuri kwenye serikali",Amesema Kibonde.


Akizungumzia vipaumbele vyake pindi atakapopata ridhaa ya wananchi kyongoza amesema chama chao kimeweka vipaumbele vitatu ambayo ni Elimu,kilimo na afya ambapo katika elimu wanatarajia kutoa elimu bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu.


Aidha ameongeza kuwa watajenga hospitali katika kila kata na kuweka vitendea kazi lakini kutoa fursa kwa madaktari na wauguza kwenda nje ya nchi kupata uzoefu na kuja kuutumia uzoefu huo katika hospitali za hapa nchini.

Akizungumzia kilimo amesema wamejipanga kutoa heka tano kwa kila kijana pamoja na pembejeo ili wajikite kwenye kilimo lakin pia watapata na hati miliki za heka hizo ili waweze kutumia hati hizo katika kupata mikopo kutoka kwenye taasisi za mikopo zilipo.

Sambamba na hayo ameipongeza Tume huru ya uchaguzi (INEC) kwa kuvishirikisha vyama vya siasa katika kila hatua na kuwapitisha kwenye sheria zote hivyo imewapa inami ya kuwa na uchaguzi huru na haki.

Kwa upande wake mgombea mwenza Azza Haji Suleiman ametoa rai kwa vijana kuepuka kutumika katika kuvunja amani hasa kwenye kipindi hiki cha kampeni na mpaka uchaguzi mkuu Octoba 29 badala yake watumie muda huu kusikiliza sera na kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuwachagua viongozi wa chama hicho.


"Vijana niwasihi tudumishe amani na utulivu ili uchaguze uwe na amani muepuke kushawishiwa kuwa chanzo cha machafuko kwani mkumbuke pindi amani ikikosekana kuna wagonjwa wazee na watoto ndio watakao pata matatizo zaidi hivyo niwaombe muendelee kuwa mabolozi wazuri wa amani nchini",Amesema.

Naye,Katibu mkuu wa chama hicho ambae pia ni mgombea Urais kwa Serikali ya mapinduzi  Zanzibar Ameir Hassan Ameir amesema pindi watakapoingia madarakani wataanzisha mfuko wa mikopo kwa ajili ya mama lishe lengo likiwa kumkwama mwanamke kiuchumi kwani mkopo huo hautakuwa na riba.


Pia ameongeza kuwa watatoa bodaboda milioni moja bure kwa vijana lengonkuchochea ajira lakini pia kutoa mkopo wa milioni 10 kwa kila mfanyabiashara wa mitumba pamoja na kutoa posho ya laki moja kwa mwezi kwa wazee nchi nzima.






Comments

Popular posts from this blog

HAPI AWATAKA WAGOMBEA WALIOKOSA UTEUZI KUVUNJA MAKUNDI NA KUUNGANA KUTAFUTA KURA ZA KISHINDO ZA CHAMA HICHO.

Msajili Hazina aipa tano TPA

YUSUPH RAI AWASII WANANCHI TEMEKE KUCHAGUA MTU SIO CHAMA KWA MAENDELEO YA JIMBO HILO.