CHAUMA WAIOMBA INEC KUINGILIA KATI MGOGORO KATIKA JIMBO LA SEGEREA.

 


Na Mwandishi Wetu.


Chama cha CHAUMA kimeiomba Tume huru ya Uchaguzi (INEC)kuingilia kati mgogoro unaoendelea katika jimbo la Segerea ambapo kimemlalamikia mgombea ubunge jimbo la hilo kupitia chama cha Mapinduzi Bonna Kamori kwa kumtuhumu kukusanya kadi za mpiga kura kwa wananchi wa jimbo hilo jambo ambalo ni kinyume cha sheria.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 12,2025 Jijini Dar es salaam Naibu Katibu Mkuu(CHAUMA)Benson Kigaila amesema malalamiko hayo wameshayafikisha kwenye vyombo mbalimbali vya sheria ikiwemo TAKUKURU pamoja na kuandikia barua tume huru ya uchaguzi na hawakupata majibu yeyote.


"Hili swala tumeamua kulileta kwenye umma ili tuweze kusaidiana maana kwenye mamlaka husika tumeshalipeleka na hakuna majibu yoyote kwamba ni hatua gani zinachukuliwa",Amesema.

Ameongeza kuwa kitendo hiko kinachofanywa ni kuuharifu uchaguzi kwani kukusanya shahada za mpiga kura ni kinyume cha sheria kwani kuzikusanya ni hujuma kwani unaweza kupelekea watu wakashindwa kupiga kura.


Aidha Kigaila amemtaja mwalimu mmoja(jina limehifadhiwa) wa shule ya sekondari Bonyokwa ametajwa kuhusika na ukusanyaji wa vitambulisho vya wanafunzi ambao wamejiandikisha kupiga kura.


"Tunataka hatua zichukuliwe na watu warudushiwe shahada zao na waliojihusisha na udanganyifu huo wachukuliwe hatua za kisheria",Amesema.



Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi waliokutana na kadhia hiyo wamesema Tume unapaswa kuongilia kati jambo hilo ili uchaguzi uwe huru na haki.


Filbert Werema mgombea udiwani kata ya Kisukuru amesema baada tu yakufunguliwa tu kwa kampeni zoezi hilo lilianza katika kata yake na taarifa amekuwa akifikishiwa kwa njia mbalimbali ikiwemo kupigiwa simu.


Modester Dismas Kata ya kipawa muhanga wa kuchukuliwa kitambulisho na mpaka sasa kitambulisho hiko hakijamfikia na hajui hatima yake na wenzie 25 ambao wamechukuliwa vitambulisho hivyo.


Muandishi wa habari hii alimtafuta mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Segerea Bonna Kamori na kukataa kuzungumzia swala hilo huku akidai tuhuma hizo hazina ukweli.


Nae Mwalimu wa shule ya Sekondari Bonyokwa ambae anatuhumiwa kuchukua vitambulisho vya wanafunzi akizungumza kwa njia ya simu amesema tuhuma hizo si za kweli na badala yake amehitaji wanaomtuhumu kuonyesha udhibitisho wa Tuhuma hizo.






Comments

Popular posts from this blog

HAPI AWATAKA WAGOMBEA WALIOKOSA UTEUZI KUVUNJA MAKUNDI NA KUUNGANA KUTAFUTA KURA ZA KISHINDO ZA CHAMA HICHO.

Msajili Hazina aipa tano TPA

YUSUPH RAI AWASII WANANCHI TEMEKE KUCHAGUA MTU SIO CHAMA KWA MAENDELEO YA JIMBO HILO.