CRDB YATOA GARI LINGINE KWA MSHINDI WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA HIYO.

 


Na Sophia Kingimali.


WATANZANIA wametakiwa kushiriki katika shindano la kidigital la huduma za kifedha ili kuweza kuibuka washindi na kubadilisha historia za maisha yao lakini pia kukuza matumizi fedha kidigital.


Pia,wanafunzi wa vyuo wametakiwa kutumia huduma za simbanking ili kuweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo ufadhili wa masomo na fedha taslimu.


Fahad Soud, MKAZI wa Jiji la Tanga,ameibuka mshindi wa pili wa gari jipya aina ya IST kupitia kampeni ya Benki ya CRDB inayolenga kuhamasisha matumizi ya huduma za kidijitali, hususan SimBanking.


Akizungumza katika Hafla ya makabidhiano ya zawadi hiyo ilifanyika katika Viwanja vya Dar Village, Mikocheni jijini Dar es Salaam ambapo ilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa benki hiyo na wadau mbalimbali,Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa CRDB, Stephen Adili, amesema kampeni hiyo ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa wateja wanaotumia huduma za kidijitali za benki hiyo.

“Mbali na magari aina ya IST yanayotolewa kila mwezi, zawadi nyingine mbalimbali kama fedha taslimu pia zinapatikana. Ili kushiriki, mteja anatakiwa kuwa na akaunti ya CRDB na amejiunga na SimBanking. Kila muamala unakupa nafasi ya kushinda, iwe ni kununua umeme, kulipia bili au kukata tiketi za SGR,” amesema Adili.

Adili amesisitiza kuwa huduma ya SimBanking ni jumuishi na haina mipaka kwa kundi maalumu la wateja, kwani inawahusu makundi yote wakimo wanafunzi, wafanyabiashara, watumishi wa umma na hata wafanyakazi binafsi.

Kwa upande wake, mshindi wa zawadi hiyo, Fahad Soud, aliishukuru Benki ya CRDB kwa kuendesha kampeni hiyo na kuwataka wateja wengine kujitokeza kwa wingi kutumia SimBanking.


“Nimefurahi sana kushinda gari kupitia huduma hii. Naomba Watanzania waamini kwamba kampeni hii ni ya kweli na washiriki kwa kufanya miamala kupitia SimBanking ili nao waweze kushinda kama mimi,” alisema Fahad.


Kwa mujibu wa CRDB, droo hiyo itaendelea hadi mwezi Disemba ambapo mshindi wa mwisho atajinyakulia gari aina ya Harrier Anaconda, huku wateja wengine wakiendelea kujipatia zawadi mbalimbali kila mwezi.









Comments

Popular posts from this blog

HAPI AWATAKA WAGOMBEA WALIOKOSA UTEUZI KUVUNJA MAKUNDI NA KUUNGANA KUTAFUTA KURA ZA KISHINDO ZA CHAMA HICHO.

Msajili Hazina aipa tano TPA

YUSUPH RAI AWASII WANANCHI TEMEKE KUCHAGUA MTU SIO CHAMA KWA MAENDELEO YA JIMBO HILO.