DK.NCHIMBI AENDELEA KUINADI ILANI UCHAGUZI MKUU, KUOMBA KURA ZA KISHINDO KWA CCM




Na Mwandishi Wetu,Katavi


MGOMBEA Mwenza wa Urais wa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, ameendelea kunadi Ilani ya  Chama hicho ya Uchaguzi Mkuu 2025-2030,ambayo kimsingi imelenga kwenda kuboresha maisha ya wananchi na ustawi wa maendeleo katika miaka mitano ijayo.


Dk.Nchimbi leo Septemba 9,2025 amewasili mkoani Katavi  na kuhutubia wananchi  katika Uwanja wa Maridadi,Mpanda mjini, kwenye mkutano wake wa hadhara wa Kampeni akitokea mkoani Rukwa.


Baada ya kuwahutubia Wananchi wa Mpanda Mjini,Balozi Nchimbi amewanadi  Wagombea Ubunge wa majimbo mbalimbali ya  Mkoa huo,akiwemo Mbunge wa jimbo la Mpanda mjini, Haidary Hemed Sumry pamoja na Madiwani.


Awali, Dkt Nchimbi amewahutubia wananchi wa Majimoto,katika jimbo la Kavuu mkoani Katavi na kumnadi Mgombea Ubunge wa jimbo hilo Laurent Deogratius Luswetula pamoja na Madiwani.


Akiwa katika mkutano huo Dk.Nchimbi ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua mgombea Urais wa CCM Dk.Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wa Chama hicho kwa kura za kishindo ifikapo Oktoba 29,2025







Comments

Popular posts from this blog

HAPI AWATAKA WAGOMBEA WALIOKOSA UTEUZI KUVUNJA MAKUNDI NA KUUNGANA KUTAFUTA KURA ZA KISHINDO ZA CHAMA HICHO.

Msajili Hazina aipa tano TPA

YUSUPH RAI AWASII WANANCHI TEMEKE KUCHAGUA MTU SIO CHAMA KWA MAENDELEO YA JIMBO HILO.