MIRUMBE AZINDUA KAMPENI RORYA ATAJA MIRADI YA MAENDELEO ILIYOTEKELEZWA NA SERIKALI YA CCM



Na Mwandishi wetu Rorya.


Katibu wa NEC Uchumi na Fedha na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Ndugu *Joshua Mirumbe*, azindua kampeni za Ubunge Jimbo la Rorya - Mkoani Mara


Akiongea na wananchi Mirumbe asema “Rorya Dkt Samia ameleta maendeleo makubwa katika Sekta ya Maji. Mradi wa maji Komuge, Shirati na mradi wa maji Nyamagaro hadi Tarime unaogharimu zaidi ya billion 100."


Aidha Dkt Samia Suluhu Hassani ameahidi kuwa akichaguliwa ataongeza ajira kwa walimu, kubresha huduma za afya kwakutumia Bima ya Afya kwa wote na kukuza Uchumi wa Taifa kwa kukamilisha Miundombinu ya kuchechemua uchumi kama Reli ya SGR toka Dodoma Marampaka  hadi Mwanza na kipande cha Isaka hadi Burundi - asema Mirumbe


Aidha Mirumbe amewasistiza wana CCM na wananchi wa Rorya kuendelea kuiamini CCM nakuichagua kwani ndicho chama chenye Ilani inayotekelezeka na Kuomba ifikapo tarehe 29 October 2025 wamchangue Dkt Samia Suluhu Hassani nafasi ya Rais na Balozi Dkt Emanuel Nchimbi Mgombea Mwenza, Mbunge Ndugu  Jafari Wambura Chege na Madiwani wa CCM kata 26

Comments

Popular posts from this blog

HAPI AWATAKA WAGOMBEA WALIOKOSA UTEUZI KUVUNJA MAKUNDI NA KUUNGANA KUTAFUTA KURA ZA KISHINDO ZA CHAMA HICHO.

Msajili Hazina aipa tano TPA

YUSUPH RAI AWASII WANANCHI TEMEKE KUCHAGUA MTU SIO CHAMA KWA MAENDELEO YA JIMBO HILO.