HAPI AWATAKA WAGOMBEA WALIOKOSA UTEUZI KUVUNJA MAKUNDI NA KUUNGANA KUTAFUTA KURA ZA KISHINDO ZA CHAMA HICHO.
Na.Mwandishi Wetu. KATIBU Mkuu Jumuiya ya Wazazi(CCM) Ally Hapi (MNEC)amewataka wagombea ambao hawakupata uteuzi ndani ya chama kuungana na kukitafutia chama na wagombea wake kura za kishindo ili chama kiendelee kushika dola Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Septemba 13, 2025 amezindua rasmi kampeni za Ubunge Jimbo la Kinondoni zilizofanyika uwanja wa Mwinjuma Kata ya Kinondoni Dar es Salaam Hapi amewashukuru Wanançhi Kinondoni kwa kujitokeza kwa wingi ambapo amewahakikishia kuwa wamepata mtu sahihi na mchapakazi, mnyenyekevu, anajishusha kwa watu wote wa juu na chini huku akiwataka kutokuwa na mashaka nae. "Nimewahi fanya kazi hapa Kinondoni kama Mkuu wa Wilaya, nafahamu uwezo wa Mgombea wetu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Kinondoni Mheshimiwa Tarimba na sina shaka nae kabisa mpeni kura nyingi za Ndiyo Oktoba 29 na pia kwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan na Madiwani wote kutoka CCM. Tuvunje makundi, na sasa tukunjue mioyo tutafute kura kwa Mbunge, Rais na Diwani...



Comments
Post a Comment