WAZIRI WA KAZI NA UWEKEZAJI ZANZIBAR ASIFU TUZO ZA WATENDAJI AZITAJA KUWA KIVUTIO CHA UWEKEZAJI.
Na Mwandishi Wetu.
Waziri wa Kazi na Uwekezaji Zanzibar, Shariff Ali Shariff Asema tuzo za Wakuu na Watendaji wa Makampuni 100 Bora Kuvutia Uwekezaji na kukuza uchumi wa Tanzannia.
Waziri Shariff aliyasema hayo wakati akishiriki hafla ya utoaji tuzo hizo zilizofanyika 21 Novemba 2025 katika ukumbi wa The Super Dome Masaki Dar es salaam na kuhudhuliwa na watendaji mbalimbali
"Tuzo hizi zimekuwa kivutio kikubwa cha uwekezaji nchini hali inayopelekea uchumi wetu kama nchi kukua lakini na utendaji kazi wa makampuni mbalimbali kuimalika",Amesema Shariff.



Comments
Post a Comment