BoT yaimarisha usimamizi wa akiba ya taifa, yauza ziada ya dhahabu kupunguza vihatarishi

Na.Mwandishi Wetu.

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeeleza kuwa hatua ya kuuza sehemu ya dhahabu iliyopo kwenye hifadhi yake inalenga kuimarisha usimamizi wa akiba ya taifa na kupunguza vihatarishi vya kifedha, badala ya kufadhili miradi ya maendeleo ya serikali kama ilivyodhaniwa na baadhi ya wadau.

Akizungumza na waandishi wa habari leo January 30,2026  jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Masoko ya Fedha wa BoT, Emmanuel Akaro, amesema Bodi ya Benki hiyo imeweka kiwango cha juu cha hifadhi ya dhahabu kisichozidi thamani ya Dola za Marekani bilioni mbili, huku kiwango cha sasa kikiwa kimefikia takribani dola bilioni 3.2.

Akaro amesema ziada hiyo ndiyo inayopangwa kuuzwa ili kurejesha uwiano sahihi wa muundo wa hifadhi ya fedha za kigeni, hatua inayolenga kuhakikisha akiba ya taifa inabaki salama na inayoweza kutoa faida kupitia uwekezaji wa kimataifa.

Amefafanua kuwa fedha zitakazopatikana zitawekezwa kwenye masoko ya fedha ya kimataifa ili kuongeza mapato ya uwekezaji wa BoT, na kusisitiza kuwa matumizi ya fedha za benki kuu kwa ajili ya serikali lazima yaidhinishwe na Bunge.

Amesema uamuzi huo ni sehemu ya mkakati wa kudhibiti vihatarishi, akieleza kuwa BoT inapouza dhahabu hununua Dola za Marekani ili kusawazisha mchanganyiko wa hifadhi na kuepuka hatari ya kutegemea mali aina moja pekee.

Ameongeza kuwa hadi Januari 29, 2025, Tanzania ilikuwa na akiba ya fedha za kigeni yenye thamani ya dola bilioni 6.5, ikijumuisha dhahabu, Dola za Marekani na sarafu ya China, hali inayoonesha uimara wa nafasi ya nchi katika kukabiliana na misukosuko ya kiuchumi ya kimataifa.

Akaro amesema BoT inaendelea kununua dhahabu ya ndani kama sehemu ya kuunga mkono sekta ya madini, huku ikinunua wastani wa tani mbili kwa mwezi, sawa na asilimia 20 ya dhahabu inayozalishwa nchini.

Amesisitiza kuwa pamoja na mauzo ya dhahabu, BoT itaendelea kuingiza fedha za kigeni kwenye soko la ndani ili kusaidia uthabiti wa thamani ya Shilingi ya Tanzania na kuhakikisha upatikanaji wa fedha za kigeni kwa wananchi na serikali.iyo inayopangwa kuuzwa ili kurejesha uwiano sahihi wa muundo wa hifadhi ya fedha za kigeni, hatua inayolenga kuhakikisha akiba ya taifa inabaki salama na inayoweza kutoa faida kupitia uwekezaji wa kimataifa.

Amefafanua kuwa fedha zitakazopatikana zitawekezwa kwenye masoko ya fedha ya kimataifa ili kuongeza mapato ya uwekezaji wa BoT, na kusisitiza kuwa matumizi ya fedha za benki kuu kwa ajili ya serikali lazima yaidhinishwe na Bunge.

Aidha Akaro ameongeza kuwa, uamuzi huo ni sehemu ya mkakati wa kudhibiti vihatarishi, akieleza kuwa BoT inapouza dhahabu hununua Dola za Marekani ili kusawazisha mchanganyiko wa hifadhi na kuepuka hatari ya kutegemea mali aina moja pekee.

Ameongeza kuwa hadi Januari 29, 2025, Tanzania ilikuwa na akiba ya fedha za kigeni yenye thamani ya dola bilioni 6.5, ikijumuisha dhahabu, Dola za Marekani na sarafu ya China, hali inayoonesha uimara wa nafasi ya nchi katika kukabiliana na misukosuko ya kiuchumi ya kimataifa.

Akaro amesema BoT inaendelea kununua dhahabu ya ndani kama sehemu ya kuunga mkono sekta ya madini, huku ikinunua wastani wa tani mbili kwa mwezi, sawa na asilimia 20 ya dhahabu inayozalishwa nchini.

Amesisitiza kuwa pamoja na mauzo ya dhahabu, BoT itaendelea kuingiza fedha za kigeni kwenye soko la ndani ili kusaidia uthabiti wa thamani ya Shilingi ya Tanzania na kuhakikisha upatikanaji wa fedha za kigeni kwa wananchi na serikali.

Comments

Popular posts from this blog

HAPI AWATAKA WAGOMBEA WALIOKOSA UTEUZI KUVUNJA MAKUNDI NA KUUNGANA KUTAFUTA KURA ZA KISHINDO ZA CHAMA HICHO.

Msajili Hazina aipa tano TPA

YUSUPH RAI AWASII WANANCHI TEMEKE KUCHAGUA MTU SIO CHAMA KWA MAENDELEO YA JIMBO HILO.