FURAHA KWA WATEJA CRDB: WASHINDA SAFARI YA KOMBE LA DUNIA 2026, WENGINE WATINGA NA TV ZA KISASA INCHI 85.

 


Na Mwandishi Wetu

Furaha na shangwe vimetawala kwa baadhi ya Watanzania baada ya kujikuta wakishinda zawadi nono kupitia kampeni ya “Tembo Card Visa” ya Benki ya CRDB, huku wanne wakipata nafasi ya kipekee ya kusafiri kwenda Marekani kushuhudia fainali za Kombe la Dunia 2026.

Washindi hao, waliopatikana kupitia droo ya kwanza iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam, wameeleza hisia zao za mshangao na furaha, wakisema hawakutarajia kupata nafasi hiyo adhimu katika maisha yao.

Miongoni mwa washindi wa safari hiyo ni Kenneth Masana Bina kutoka Kagera, Gasper Melkiory Kavishe wa Morogoro, pamoja na wakazi wa Dar es Salaam Arnold John Samugabo na Erick Harison Mlinga.

Mbali na safari hiyo ya kihistoria, washindi wengine watatu walijishindia runinga janja (Smart TV) za inchi 85 pamoja na dishi na kifushi, wakisema zawadi hizo zitabadilisha namna wanavyofurahia burudani majumbani mwao.

Akizungumza mara baada ya droo hiyo, Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Kadi wa CRDB, Karington Chahe, amesema kampeni hiyo inalenga kuwagusa moja kwa moja wateja kwa kuwapa zawadi zenye thamani huku ikiendelea kuhamasisha matumizi ya kadi.

“Leo tumeshuhudia furaha ya kweli kwa wateja wetu. Hii ni sehemu ya kuwashukuru na kuwapa motisha zaidi,” amesema.

Baadhi ya washindi walieleza kuwa ushindi huo umekuwa wa kushtukiza, huku wakiahidi kuendelea kutumia huduma za kadi katika miamala yao ya kila siku.

Kwa mujibu wa CRDB, kampeni hiyo iliyoanza Machi 12, 2026, itaendelea hadi Juni mwaka huu, ambapo washindi zaidi wanatarajiwa kupatikana, wakiwemo watakaosafiri kwenda kushuhudia moja ya mashindano makubwa zaidi ya soka duniani.

Kwa wengi wa washindi, zawadi hizo si tu zawadi za kawaida, bali ni ndoto zilizotimia—hasa kwa wale watakaopata nafasi ya kushuhudia Kombe la Dunia ana kwa ana kwa mara ya kwanza maishani mwao.

Comments

Popular posts from this blog

HAPI AWATAKA WAGOMBEA WALIOKOSA UTEUZI KUVUNJA MAKUNDI NA KUUNGANA KUTAFUTA KURA ZA KISHINDO ZA CHAMA HICHO.

Msajili Hazina aipa tano TPA

YUSUPH RAI AWASII WANANCHI TEMEKE KUCHAGUA MTU SIO CHAMA KWA MAENDELEO YA JIMBO HILO.