KATIBU MKUU MATARAGIO AIPONGEZA PBPA KWA KUHAKIKISHA UWEPO WA MAFUTA YA KUTOSHA NCHINI



Na.Mwandishi wetu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati (anayeshughulikia mafuta na gesi),Dkt. James Mataragio ameipongeza Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA) kwa kuhakikisha nchi inakuwa na mafuta ya kutosha wakati wote.

Ameyasema hayo leo Aprili 21,2026 alipotembelea Banda la PBPA katika Maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.


 Akifafanua wakati wa ziara hiyo, Meneja wa Sheria, Bi. Lilian Rwegimbura amesema mpaka sasa mafuta yapo ya kutosha na ambayo yapo melini ni metriki tani lita milioni 42 hivyo PBPA inaendelea kuhakikisha upatikanaji wa uhakika wa mafuta.

Comments

Popular posts from this blog

Kafulila: Familia Ndogo, Uchumi Imara Ndiyo Njia ya Tanzania Kufikia Maendeleo

WANAHABARI WATAKIWA KUJIUNGA VYAMA VYA WAFANYAKAZI KULINDA HAKI ZAO

MRADI WA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME CHALINZE–DODOMA KUKAMILIKA AGOSTI 2026 : MD TWANGE