Watanzania waaswa kudumisha amani ili kumtukuza Mungu.

 


Na. Mwandishi wetu.

Watanzania wameaswa kudumisha amani na mshikamano kuelekea sikukuu ya pasaka ili kuupokea ufufuko wa yesu kristu kwa roho na kweli

Wakati akitoa salamu za pasaka Askofu wa kanisa la WRC ( The word ofvReconciliation church) Askofu Nicklous Siguye Amesema kuwa watanzania ni watu wenye utamaduni wa upole na kupenda amani

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa kama nchi tunapashwa kuwa wamoja bila kujali itikadi za kidini, kisiasa na kikabila ili kuijenga nchi iliyo na umoja

Lakini pia amewataka waamini kujiungamanisha na yesu kristu kwa siku zilizo baki kuanzia leo ijumaa kuu mpaka kufikia pasaka ufufuko wa yesu kristu

Jumatatu ya pasaka itakuwa ni siku ya maadhimisho ya miaka 19 ya kanisa la WRC ( The word of Reconciliation Church) na kuwakaribisha Watanzania wote kushiriki kwa pamoja kumtukuza Mungu 

Comments

Popular posts from this blog

HAPI AWATAKA WAGOMBEA WALIOKOSA UTEUZI KUVUNJA MAKUNDI NA KUUNGANA KUTAFUTA KURA ZA KISHINDO ZA CHAMA HICHO.

Msajili Hazina aipa tano TPA

YUSUPH RAI AWASII WANANCHI TEMEKE KUCHAGUA MTU SIO CHAMA KWA MAENDELEO YA JIMBO HILO.