TANESCO YAENDELEA KUWAELIMISHA WANAOFANYA SHUGHULI ZA KIUCHUMI KWENYE MIUNDOMBINU YA UMEME
📌Ni katika muendelezo wa ukaguzi wa miundombinu ya umeme Dar es salaam 📌Yatoa rai kwa wananchi kuondoka kwa ajili ya usalama wa maisha na mali zao Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeendelea kuwasisitiza wananchi wanaofanya shughuli zao za kiuchumi katika miundombinu ya umeme kuondoka katika maeneo hayo kwa hiari, kwa kuwa wanahatarisha usalama wa maisha na mali zao. Akizungumza katika muendelezo wa zoezi la kukagua miundombinu ya umeme Mei 18, katika eneo la Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam, Msimamizi Msaidizi wa Njia Kuu za Kusafirisha Umeme Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Nicholaus Kivelege, amesema TANESCO inafanya jitihada za makusudi kutoa elimu kuhusu athari za kuendelea kufanya shughuli za kiuchumi chini ya njia kubwa za kusafirisha umeme katika maeneo mbalimbali nchini. Amesema licha ya jitihada hizo, bado baadhi ya wananchi wanaendelea kufanya shughuli hizo, hivyo amewaomba viongozi wa serikali za mitaa katika maeneo husika kuongeza nguvu ya kutoa elimu kuhusu madhara ya...