Posts

MCHANGE AHOJI: DK. NCHIMBI ANAJUA MADHARA YA KAULI ZAKE AU ANATUTEGA?

Image
  Na Mwandishi Wetu Mchambuzi wa masuala ya siasa, jamii na maendeleo, Habibu Mchange, ametoa tafakuri kuhusu utata wa kauli za mara kwa mara za Makamu wa Rais, Dk. Emmanuel Nchimbi, akisema kutokana na nafasi yake ya kikatiba kama Msaidizi Mkuu wa Rais kwa mujibu wa Ibara ya 47(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kauli zake zinapaswa kupimwa kwa uzito mkubwa kwa kuwa zina athari kwa Serikali, mshikamano wa uongozi na imani ya wananchi kwa taasisi za dola. Katika tafakuri hiyo yenye kichwa "DK. NCHIMBI ANAJUA MADHARA YA KAULI ZAKE AU ANATUTEGA?", Mchange amechambua kauli ya Dk. Nchimbi kwamba "Katiba iliyopo ina mapungufu na inampa Rais madaraka yasiyo na maana," pamoja na wito wake wa "komaeni, pambaneni mpate Katiba mpya," akisema kauli hizo zimezua mjadala mkubwa wa kikatiba na kisiasa, hasa wakati Serikali tayari imeeleza kuwa mchakato wa Katiba mpya utaanza baada ya kukamilika kwa maridhiano ya kitaifa.  Amehoji kuwa iwapo Serikali tayari...

UMEME JUA KISHAPU AWAMU YA PILI KUIONGEZEA TANZANIA MEGAWATI 100 ZA NISHATI JADIDIFU

Image
📌Waziri Ndejembi ashuhudia utiaji saini, asema ni alama ya miradi ya kielelezo nchini. 📌Mradi utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 100   📌Aeleza mradi kugharimu Shilingi bilioni 204.4 na kuchochea sekta za kilimo, viwanda na uchimbaji wa madini.   📌Aitaka TANESCO kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mradi ili ukamilike kwa wakati. Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imeingia hatua mpya ya kuongeza vyanzo vya uzalishaji umeme baada ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa awamu ya pili ya Mradi wa umeme kwa nguvu ya Jua Kishapu utakaozalisha jumla ya megawati 100. Hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha jumla ya megawati 50 na kuingizwa katika Gridi ya Taifa, jambo lililoongeza uwezo na uthabiti wa gridi hiyo na kuimarisha upatikanaji wa umeme katika maeneo mbalimbali nchini. Akizungumza katika hafla hiyo Julai 27, 2026, Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema sekta ya nishati ni mhimili wa ...

Taasisi za Umma zatakiwa kutokuwa kikwazo kwa wawekezaji

Image
Na Mwandishi wa OTR Pwani. Serikali imezitaka Taasisi za Umma kuhakikisha zinakuwa chachu ya ukuaji wa uchumi kwa kutengeneza mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji kupitia mifumo yenye ufanisi, kupunguza urasimu usio wa lazima, kuboresha utoaji wa huduma na kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi katika kuunga mkono utekelezaji wa Dira 2050. Wito huo ulitolewa Julai 24,2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, wakati akifunga awamu ya tatu ya Programu ya Mafunzo Elekezi ya siku nne kwa Watendaji Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha mkoani Pwani. Akizungumza na viongozi hao, Mhe. Kikwete alisema mafanikio ya Dira 2050 hayatategemea ubora wa sera na mipango pekee, bali namna taasisi za umma zitakavyotekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuzalisha matokeo yanayoonekana kwa wananchi na kwa uchumi wa Taifa. Amewataka Wakuu wa Taasisi za Umma ku...

Taasisi za umma zatakiwa kuachana na utendaji wa mazoea ili kufanikisha Dira 2050

Image
  Na Mwandishi wa OTR Pwani. Serikali imezitaka Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali kuachana na utendaji wa mazoea na kujielekeza katika uongozi unaozingatia matokeo, ubunifu, uwajibikaji na ushirikiano wa karibu na sekta binafsi ili kuharakisha utekelezaji wa DIRA ya Taifa ya Maendeleo 2050. Wito huo ulitolewa Jumanne jioni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, wakati akifungua Mafunzo Elekezi kwa Watendaji Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali yanayoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Taasisi ya UONGOZI katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha mkoani Pwani. Mafunzo hayo ya siku nne yanafanyika chini ya kaulimbiu "Kutoka Maono mpaka Matokeo: Kufungamanisha Utendaji wa Mashirika ya Umma na DIRA 2050."   Akizungumza katika hafla hiyo, Prof. Mkumbo alisema Tanzania imeweka lengo la kufikia uchumi wa kati wa juu na kukuza Pato la Taifa (GDP) kutoka dola za Ma...

WAZIRI NDEJEMBI ATOA ONYO KWA MKANDARASI ANAYETEKELEZA MRADI WA SONGEA–TUNDURU–MASASI

Image
  📌 Asema ucheleweshaji wa mradi hauendani na matarajio ya Serikali na wananchi. 📌 Amuagiza mkandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji na kuzingatia masharti ya mkataba. 📌 Aelekeza hatua stahiki kuchukuliwa iwapo maendeleo ya mradi hayataboreshwa kabla ya Septemba 30, 2026. 📌 Mradi wa kV 220 utaiunganisha Mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye Gridi ya Taifa na kuimarisha upatikanaji wa umeme Kusini mwa Tanzania. 📍Tunduru, Ruvuma  Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameonesha kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme wa msongo wa kilovoti 220 kutoka Songea hadi Masasi kupitia Tunduru na kuagiza mkandarasi kuongeza juhudi ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati uliopangwa. Akizungumza wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo leo Julai 22, 2026, Mhe. Ndejembi amesema Serikali haitakuwa tayari kuona miradi ya kimkakati inayogusa maisha ya wananchi ikicheleweshwa bila sababu za msingi. Amesema mradi huo ni miongoni mwa miradi muhimu...

NEWALA KUNUFAIKA NA UMEME WA UHAKIKA.

Image
  📌*Ni baada ya kukamilika kwa njia ya kusafirisha umeme ya kilovoti 33 Masasi - Mtwara* 📌*Mradi umeimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi wa Wilaya ya Newala na maeneo jirani.* 📌*MD Twange asema thamani ya mradi ni takribani shilingi bilioni 4.65* 📍Newala, Mtwara | Julai 21, 2026 Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amezindua rasmi mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovoti 33 kutoka Masasi hadi Newala, akieleza kuwa mradi huo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuendelea kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi na kuweka mazingira wezeshi kwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika Wilaya ya Newala. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa njia hiyo, Mhe. Ndejembi amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kuwekeza katika miradi ya kimkakati ya umeme ili kuhakikisha huduma ya nishati inawafikia wananchi wengi zaidi na kuwa chachu ya maendel...

SUA yaipongeza PPPC kwa kukuza ajenda ya ubia katika sekta ya kilimo

Image
  Na.Mwandishi wetu.  Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimepongeza Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta ya Binafsi (PPPC) kwa kuendelea kuhamasisha matumizi ya ubia (PPP) kama nyenzo ya kuharakisha maendeleo ya sekta ya kilimo na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa. Akizungumza leo July 17,2026 wakati wa Mhadhara wa Wazi kwa Umma ulioandaliwa na PPPC katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Naibu Makamu Mkuu wa SUA, Prof. Amandus Muhairwa, alisema uamuzi wa PPPC kuandaa mhadhara huo chuoni hapo unaonesha kutambua nafasi ya kimkakati ya kilimo katika kufanikisha ajenda ya maendeleo ya Tanzania. Alisema SUA imefarijika kuwa miongoni mwa taasisi za elimu ya juu zinazoshirikishwa katika mijadala kuhusu ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, akibainisha kuwa ushirikiano huo ni hatua muhimu katika kuunganisha elimu, utafiti, ubunifu na uwekezaji kwa ajili ya maendeleo ya Taifa. "Tunayo heshima kubwa kumpokea Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC, Bw. David Kafulila, pam...