Posts

Msajili wa Hazina, Fitch Ratings watathmini mageuzi ya taasisi za umma

Image
  Na Mwandishi wa OTR Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) Jumanne, Agosti 11, 2026, ilifanya mazungumzo na kampuni ya Fitch Ratings Ltd ikiwa ni sehemu ya mapitio ya pili ya mwaka 2026 ya tathmini ya Fitch Ratings, katika mchakato unaohusisha taasisi mbalimbali za Serikali. Mazungumzo hayo yanalenga  kuwapa wachambuzi wa Fitch Ratings fursa ya kupata taarifa za kina kuhusu mwenendo wa uchumi wa Tanzania, utekelezaji wa sera za kibajeti na fedha, pamoja na mikakati ya Serikali katika usimamizi wa deni la Taifa.  Kwa upande wa OTR, mjadala ulijikita katika utendaji wa taasisi za umma, mageuzi yanayoendelea, vihatarishi vya kifedha, pamoja na mtiririko wa fedha kati ya Serikali na taasisi za Umma. Mapema mwaka huu, Fitch Ratings iliendelea kuipa Tanzania daraja ‘B+’ kwa hadhi ya ulipaji wa madeni ya muda mrefu ya fedha za kigeni, ikitaja mwelekeo imara wa ukuaji wa uchumi na uwezo wa Serikali kukabiliana na changamoto za kifedha baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 20...

Taasisi 54 za Umma kuwasilisha taarifa za utendaji wa uwekezaji bungeni

Image
  Dodoma. Jumla ya taasisi za umma 54 zinatarajiwa kuwasilisha taarifa za utendaji wa uwekezaji mbele ya Kamati za Kudumu za Bunge kwa muda wa wiki tatu, katika mchakato unaolenga kuwezesha uchambuzi wa thamani na utendaji wa mitaji ya umma pamoja na utekelezaji wa mipango ya kimkakati ya taasisi husika. Katika awamu hii iliyoanza Jumatatu, Agosti 3, 2026, taasisi hizo zimepangwa kuwasilisha taarifa zao mbele ya Kamati mbili za Kudumu za Bunge, ambapo 27 zitawasilisha mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) na nyingine 27 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Umma (PAC). Hadi Jumatano, Agosti 5, 2026, taasisi nne zilikuwa tayari zimewasilisha taarifa zao mbele ya Kamati.  Taasisi hizo ni Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) na Wakala wa Huduma za Ununuzi Serikalini (GPSA), huku Kamati zikionesha kuridhishwa na utendaji wa taasisi husika. Uwasilish...

KITUO CHA UBIA CHAKUTANA NA WANAHABARI KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS.

Image
  • Ni katika kusukuma mkakati wa uchumi wa Dola trilioni moja Na Mwandishi Wetu. DAR ES SALAAM. Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPPC), David Kafulila, ameanza kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukutana na waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii ili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050. Kikao hicho cha kimkakati kilichofanyika Jumanne, Agosti 4, 2026, katika ofisi za PPPC jijini Dar es Salaam. Kafulila amekutana na waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii siku moja baada ya Rais Samia kutangaza, wakati wa uzinduzi wa nyenzo za utekelezaji wa Dira 2050 uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam, kuwa nchi sasa inaingia katika hatua ya utekelezaji wa vitendo na kwamba muda wa maneno umekwisha. Katika kikao hicho, Kafulila amesema hatua ya kukutana na wamiliki na waandishi wa majukwaa ya kidijitali inalenga kutekeleza agizo la moja kwa moja la Rais Samia, aliyezitaka taasisi za umma kutoa elimu kwa wana...

MCHANGE AHOJI: DK. NCHIMBI ANAJUA MADHARA YA KAULI ZAKE AU ANATUTEGA?

Image
  Na Mwandishi Wetu Mchambuzi wa masuala ya siasa, jamii na maendeleo, Habibu Mchange, ametoa tafakuri kuhusu utata wa kauli za mara kwa mara za Makamu wa Rais, Dk. Emmanuel Nchimbi, akisema kutokana na nafasi yake ya kikatiba kama Msaidizi Mkuu wa Rais kwa mujibu wa Ibara ya 47(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kauli zake zinapaswa kupimwa kwa uzito mkubwa kwa kuwa zina athari kwa Serikali, mshikamano wa uongozi na imani ya wananchi kwa taasisi za dola. Katika tafakuri hiyo yenye kichwa "DK. NCHIMBI ANAJUA MADHARA YA KAULI ZAKE AU ANATUTEGA?", Mchange amechambua kauli ya Dk. Nchimbi kwamba "Katiba iliyopo ina mapungufu na inampa Rais madaraka yasiyo na maana," pamoja na wito wake wa "komaeni, pambaneni mpate Katiba mpya," akisema kauli hizo zimezua mjadala mkubwa wa kikatiba na kisiasa, hasa wakati Serikali tayari imeeleza kuwa mchakato wa Katiba mpya utaanza baada ya kukamilika kwa maridhiano ya kitaifa.  Amehoji kuwa iwapo Serikali tayari...

UMEME JUA KISHAPU AWAMU YA PILI KUIONGEZEA TANZANIA MEGAWATI 100 ZA NISHATI JADIDIFU

Image
📌Waziri Ndejembi ashuhudia utiaji saini, asema ni alama ya miradi ya kielelezo nchini. 📌Mradi utakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 100   📌Aeleza mradi kugharimu Shilingi bilioni 204.4 na kuchochea sekta za kilimo, viwanda na uchimbaji wa madini.   📌Aitaka TANESCO kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mradi ili ukamilike kwa wakati. Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imeingia hatua mpya ya kuongeza vyanzo vya uzalishaji umeme baada ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa awamu ya pili ya Mradi wa umeme kwa nguvu ya Jua Kishapu utakaozalisha jumla ya megawati 100. Hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza ya mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha jumla ya megawati 50 na kuingizwa katika Gridi ya Taifa, jambo lililoongeza uwezo na uthabiti wa gridi hiyo na kuimarisha upatikanaji wa umeme katika maeneo mbalimbali nchini. Akizungumza katika hafla hiyo Julai 27, 2026, Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema sekta ya nishati ni mhimili wa ...

Taasisi za Umma zatakiwa kutokuwa kikwazo kwa wawekezaji

Image
Na Mwandishi wa OTR Pwani. Serikali imezitaka Taasisi za Umma kuhakikisha zinakuwa chachu ya ukuaji wa uchumi kwa kutengeneza mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji kupitia mifumo yenye ufanisi, kupunguza urasimu usio wa lazima, kuboresha utoaji wa huduma na kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi katika kuunga mkono utekelezaji wa Dira 2050. Wito huo ulitolewa Julai 24,2026 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete, wakati akifunga awamu ya tatu ya Programu ya Mafunzo Elekezi ya siku nne kwa Watendaji Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha mkoani Pwani. Akizungumza na viongozi hao, Mhe. Kikwete alisema mafanikio ya Dira 2050 hayatategemea ubora wa sera na mipango pekee, bali namna taasisi za umma zitakavyotekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuzalisha matokeo yanayoonekana kwa wananchi na kwa uchumi wa Taifa. Amewataka Wakuu wa Taasisi za Umma ku...

Taasisi za umma zatakiwa kuachana na utendaji wa mazoea ili kufanikisha Dira 2050

Image
  Na Mwandishi wa OTR Pwani. Serikali imezitaka Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali kuachana na utendaji wa mazoea na kujielekeza katika uongozi unaozingatia matokeo, ubunifu, uwajibikaji na ushirikiano wa karibu na sekta binafsi ili kuharakisha utekelezaji wa DIRA ya Taifa ya Maendeleo 2050. Wito huo ulitolewa Jumanne jioni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, wakati akifungua Mafunzo Elekezi kwa Watendaji Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali yanayoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Taasisi ya UONGOZI katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha mkoani Pwani. Mafunzo hayo ya siku nne yanafanyika chini ya kaulimbiu "Kutoka Maono mpaka Matokeo: Kufungamanisha Utendaji wa Mashirika ya Umma na DIRA 2050."   Akizungumza katika hafla hiyo, Prof. Mkumbo alisema Tanzania imeweka lengo la kufikia uchumi wa kati wa juu na kukuza Pato la Taifa (GDP) kutoka dola za Ma...