Kafulila: Familia Ndogo, Uchumi Imara Ndiyo Njia ya Tanzania Kufikia Maendeleo
Leo ni Siku ya Familia Duniani. Familia ndiyo taasisi ya msingi katika ujenzi wa taifa, uchumi na maendeleo ya nchi yoyote duniani. Akizungumza kupitia Mtandao wake wa kijamii wa X,Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi (PPP-CENTRE) Mhe. David Kafulila amesema moja ya changamoto kubwa zinazokabili familia nyingi nchini ni suala la uzazi wa mpango na ukubwa wa familia usioendana na uwezo wa kiuchumi wa wazazi. Hali hii husababisha ugumu wa kuwalea watoto katika mazingira bora yatakayowafanya kuwa rasilimali watu yenye ubora, uwezo wa kutimiza ndoto zao na kuchangia maendeleo ya taifa bila kutegemea Serikali kwa kiwango kikubwa. Kwa sasa, Tanzania ina kiwango cha ongezeko la watu kinachozidi asilimia 3 kwa mwaka, kiwango ambacho ni kikubwa kuliko wastani wa Bara la Afrika wa asilimia 2, pamoja na wastani wa dunia wa asilimia 1. Takwimu zinaonesha kuwa Tanzania ipo nafasi ya 81 kwa ukubwa wa uchumi duniani na nafasi ya 165 kwa pato la mtu mmoja ...


Comments
Post a Comment