WANAUME WATAKIWA KUJICHUNGUZA MARA KWA MARA UGONJWA WA SARATANI YA MATITI




Saratani ya matiti kwa wanaume imeendelea kuongezeka nchini tofauti na miaka ya nyuma ambapo idadi ya wanaume waliokuwa wakibainika kuwa na ugonjwa huo ilikuwa ndogo ambapo awali kati ya watu 100 wanaofanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti ni mwanaume mmoja pekee ndiye aliyekuwa akikutwa na saratani huku kwa sasa takwimu zikionesha kati ya watu 100 wanaume watano hubainika kuwa na saratani ya Matiti 

Akizungumza Jijini Dar es Salaam wakati wa semina kwa waandishi wa habari ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Mwezi wa Saratani Duniani Meneja wa huduma za Uchunguzi wa Saratani na Elimu kwa Umma, Dkt Maguhwa Stephan amesema saratani ya matiti imekuwa changamoto kubwa duniani, huku nchini Tanzania ikishika nafasi ya pili Duniani Kwa uwepo wa Saratani hiyo ya Matiti


Baadhi ya wahanga wa saratani ya matiti waliopata nafasi ya kushiriki semina hiyo wameeleza umuhimu wa elimu kwa jamii juu ya ugonjwa wa Saratani


Aidha Uongozi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road umetoa wito kwa Watanzania ususan wanaume kujitokeza kwa wingi kufanya uchunguzi wa saratani ya matiti na saratani nyingine kwani utambuzi wa mapema ndio silaha kuu ya kupunguza vifo vitokanavyo na ugonjwa huo

Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

HAPI AWATAKA WAGOMBEA WALIOKOSA UTEUZI KUVUNJA MAKUNDI NA KUUNGANA KUTAFUTA KURA ZA KISHINDO ZA CHAMA HICHO.

Msajili Hazina aipa tano TPA

YUSUPH RAI AWASII WANANCHI TEMEKE KUCHAGUA MTU SIO CHAMA KWA MAENDELEO YA JIMBO HILO.