MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI APEWA MAAGIZO NA BUNGE,SERIKALI

 



Na.Mwandishi wetu.

SPIKA wa Bunge Mussa Zungu amemtaka  Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Hamza Johari kuchukua   hatua kali dhidi ya Taasisi na Mashirika ambayo yalikaidi ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Utekelezaji wa Mikataba ya miradi mbalimbali kama ilivyoripotiwa na mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG 

Ameyasema hayo jana Aprili 1,2026 Bungeni Dodoma wakati wa hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu katika mwaka wa fedha 2026/27

Wakati huo huo Nae Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba amemuelekeza Mwanasheria huyo Mkuu kukaa pamoja na Wizara ya  Ardhi na TAMISEMI ili waandae mpango mkakati madhubuti katika kuhakikisha kwamba wanapata ufumbuzi wa kudumu juu ya migogoro ya ardhi inayoongezeka kila siku na kuwa kero  kwa Wananchi.

Comments

Popular posts from this blog

Kafulila: Familia Ndogo, Uchumi Imara Ndiyo Njia ya Tanzania Kufikia Maendeleo

WANAHABARI WATAKIWA KUJIUNGA VYAMA VYA WAFANYAKAZI KULINDA HAKI ZAO

MRADI WA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME CHALINZE–DODOMA KUKAMILIKA AGOSTI 2026 : MD TWANGE