Mradi wa Dola milioni 110 wa PPP, kupunguza ajali.
Na Mwandishi Wetu
MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP-CENTRE), David Kafulila, amesema kuwa mradi mkubwa wa Dola Milioni 110 kwa ajili ya ukaguzi wa usalama wa magari barabarani utaondoa adha kwa madereva.
Aidha, amesema makosa ya kibinadamu na rushwa yanayoweza kutokea wakati wa ukaguzi wa kawaida yatabainika kwa kutumia mtambo huo.
Kafulila ameyasema hay oleo Mei 13, 2026, wakati akitoa mada kwenye Warsha ya Mafunzo ya PPP kwa maafisa mbalimbali wa Serikali, inayoendelea katika jengo la PSSSF Commercial Tower, Dar es Salaam.
Alisema mradi huo umetokana na nguvu ya ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi katika matumizi ya teknolojia na kutoa suluhisho kwenye jamii.
Aidha, Mkurugenzi huyo amezitaka wizara na taasisi za serikali kuamka na kutumia rasilimali zao zilizolala, ili kuzalisha uchumi kwa kushirikiana na sekta binafsi.
Kwa mujibu wa Kafulila mfumo wa PPP unaiokoa Serikali kutumia mabilioni ya shilingi kutoka Hazina ambazo kiuhalisia hazipo, na badala yake Serikali inapata faida mara mbili.
“Tukiweza kuzitumia hizo assets ziweze kuzalisha uchumi mkubwa... tutaongeza uwezo wa serikali kufadhili miradi," alihitimisha Kafulila akiwahimiza washiriki kuchangamkia fursa hiyo.




Comments
Post a Comment