Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akizungumza leo tarehe 29 Septemba 2026 mkoani Tabora wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na Kata 11 za Tanzania bara.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akizungumza leo tarehe 29 Septemba 2026 mkoani Tabora wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma na Kata 11 za Tanzania bara.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima akizungumza jambo wakati wa mafunzo hayo.
Sehemu ya wajumbe wa Management ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.
Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Chamwino Mkoani Dodoma na Kata 11za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi**************
Na. Mwandishi Wetu, Tabora
Watendaji wa uchaguzi wamesisitizwa kuheshimu
viapo vyao na kutekeleza majukumu kwa kuzingatia Katiba, sheria na kanuni
wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Tume Huru
ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele leo
tarehe 29 Septemba, 2026 mkoani Tabora wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa
uchaguzi.
Mafunzo hayo ni sehemu ya mchakato wa
maandalizi ya uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye Jimbo la Chamwino Halmashauri ya
Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma na Kata 11 za Tanzania Bara unaotarajiwa
kufanyika tarehe 04 Novemba, 2026.
“Ninawasisitiza kuheshimu viapo vyenu kwa
nafasi mlizoteuliwa, tekelezeni majukumu yenu kwa kuzingatia Katiba ya Nchi,
sheria za uchaguzi na kanuni zake, kanuni za maadili ya uchaguzi na maelekezo
mbalimbali yanayotolewa na yatakayotolewa na Tume katika kipindi hiki cha
uchaguzi,” amesema Jaji Mwambegele.
Amewaelekeza watendaji hao kuhakikisha kuwa wakati
wote wa mchakato wa uchaguzi huo, wanavishirikisha kwa karibu vyama vyote vya
siasa vyenye usajili kamili na wadau wengine wa uchaguzi katika maeneo yao
kuhusu masuala ya kiuchaguzi ambayo wanastahili kushirikishwa.
Ameongeza kuwa watendaji hao wanapaswa kuvipatia
vyama vya siasa orodha ya vituo vya kupigia kura ili kuviwezesha kupanga
mawakala.
“Ni
muhimu kwenu pia, kuhakikisha mnayatambua na kuyajua vyema maeneo ambayo
uchaguzi utaendeshwa ikiwemo miundombinu ya kufika katika vituo vya kupigia
kura,” amesema Jaji Mwambegele.
Amewaasa watendaji hao kuhakikisha kuwa
pamoja na uzoefu ambao baadhi yao wanao katika uendeshaji wa uchaguzi, wanaepuka
kufanya kazi kwa mazoea kwa kuwa kila uchaguzi unatofautiana na uchaguzi
mwingine.
Jaji Mwambegele amewasisitiza watendaji hao
kuhakikisha wanaajiri watendaji wa vituo wenye sifa, weledi, wanaojitambua na
kuachana na upendeleo kwa ndugu na jamaa ambao hawana sifa za kufanya shughuli
za uchaguzi.
“Mhakiki vifaa vya uchaguzi mnavyopokea
kutoka Tume na kuhakikisha kila mkuu wa kituo anapata vifaa vyote vya uchaguzi
vinavyohitajika mapema na kuhakikisha siku ya uchaguzi mnaweka utaratibu
utakaowezesha kila kituo cha kupigia kura kufunguliwa saa 1:00 asubuhi,”
amesema.
Mafunzo hayo ya siku tatu yanawajumuisha waratibu
wa uchaguzi wa mikoa, wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi
ngazi ya jimbo na kata, maafisa uchaguzi, maafisa ununuzi na wahasibu.
Kata 11 za Tanzania Bara zitakazofanya
uchaguzi wa Udiwani ni Nonde iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya; Lugenge, Halmashauri
ya Mji Njombe; Bargish, Halmashauri ya Mji Mbulu; Makole, Halmashauri ya Wilaya
ya Muheza; Mwera, Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na Oldonyosambu, Halmashauri
ya Wilaya ya Ngorongoro.
Nyingine ni Igalula iliyopo Halmashauri ya
Wilaya ya Uyui; Shelui, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba; Mvumi, Halmashauri ya
Wilaya ya Kilosa; Nyarero, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na Ilolangulu, Halmashauri
ya Wilaya ya Mbogwe.
Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Chamwino Mkoani Dodoma na Kata 11za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi
Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Chamwino Mkoani Dodoma na Kata 11za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi.
Naibu Msajili na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Tabora Mhe. Gabriel Patrick Ngaeje akiwaongoza washiriki wa mafunzo kula kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa pamoja na kutunza siri wakati wakitekeleza majukumu ya Uchaguzi.
Washiriki wakila kiapo cha kujitoa uanachama na kutunza siri.
Comments
Post a Comment