TANESCO YAKAMILISHA MIRADI YA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME DODOMA.
📌 Itanufaisha wilaya za Kongwa,Gairo, Mpwapwa, na Chamwino 📌 Waziri Ndejembi azindua Kituo cha Kubadilishia Njia za Usambazaji Umeme na Transfoma ya Kudhibiti Umeme 📌 Serikali yawekeza zaidi ya Shilingi Bilioni 10.5 kuimarisha huduma ya umeme Na Mwandishi Wetu, Kongwa Wananchi wa Wilaya za Gairo, Mpwapwa, Kongwa, Chamwino na Kiteto wanatarajiwa kunufaika na huduma ya umeme wa uhakika zaidi kufuatia kukamilika kwa miradi ya kuimarisha mfumo wa usambazaji wa umeme iliyotekelezwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa gharama ya zaidi ya Shilingi bilioni 10.5. Miradi hiyo inahusisha Kituo cha Kubadilishia Njia za Usambazaji Umeme (Switching Station), Transfoma ya Kudhibiti Umeme (Automatic Voltage Regulator – AVR) yenye uwezo wa MVA 20 pamoja na njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 33 kutoka Kituo cha Kupokea na Kupoza Umeme cha Zuzu hadi Mbande yenye urefu wa kilomita 92. Akizindua miradi hiyo Juni 16, 2026 katika eneo la Mbande, Wilaya ya Kongwa, Waziri wa ...