Posts

REA, EACOP ZAINGIA MAKUBALIANO KUPELEKA UMEME JAMII PEMBEZONI MWA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA.

Image
  Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) zimeingia makubaliano yaliyolenga kufikisha umeme katika vitongoji na jamii ambazo zimepitiwa na bomba hilo la mafuta kwa upande wa Tanzania. Mkataba huo wa ushirikiano ambao utatekelezwa kwa miaka mitano, umesainiwa leo Januari 23, 2026 Jijini Dar es Salaam kati ya Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa EACOP, Guillaume Dulout. Akizungumza baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Saidy amesema kuwa makubaliano hayo yatahakikisha jamii zinazoishi pembezoni mwa mradi wa bomba la mafuta kutoka Mkoa wa Kagera mpaka Mkoa wa Tanga zinafikiwa na kunufaika na mradi huo kwa kufikishiwa huduma ya umeme. Mhandisi Saidy ameongeza kuwa ushirikiano huo pamoja na manufaa mengine unalenga kuimarisha huduma za kijamii kama shule, vituo vya afya na miradi ya maji, pamoja na kuchochea matumizi ya umeme kwa shughuli za uzalishaji m...

WATENDAJI WA UCHAGUZI PERAMIHO WATAKIWA KUVISHIRIKISHA VYAMA VYA SIASA

Image
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akizungumza leo tarehe 24 Januari, 2026 mkoani Iringa wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri za Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma na Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akizungumza leo tarehe 24 Januari, 2026 mkoani Iringa wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri za Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma na Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe. Washiriki wa mafunzo  ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri za Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma na Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya Mwemyekiti wa Tume. Washiriki wa mafunzo  ya watendaji wa uchaguzi kutoka Halmashauri za Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma na Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe wakifuatilia hotuba ya ufun...

NDEJEMBI:GHARAMA ZA UMEME HAZIJAPANDA KWA MIAKA 10

Image
  📌*Lengo ni Wananchi wamudu gharama za matumizi ya umeme* Na Mwandishi Wetu, Dodoma Licha ya kuongezeka kwa gharama za vifaa vya umeme ikiwemo nguzo, waya na mita, Serikali imeendelea kuhakikisha gharama za matumizi ya umeme kwa wananchi hazipandi kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2016. Akizungumza Januari 21, 2026 jijini Dodoma katika kikao cha pili kati ya Wizara ya Nishati, taasisi zake na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema hatua hiyo imelenga kila mwananchi apate  huduma ya umeme kwa gharama nafuu. Amesema kiwango cha uunganishaji wa umeme nchini kimefikia asilimia 52, huku Serikali ya Awamu ya Sita ikiweka lengo la kufikia asilimia 75 ifikapo mwaka 2030 linalotekelezwa kupitia Mpango wa Nishati uliosainiwa Januari 2025 wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika. Akizungumzia suala la mita janja, Waziri Ndejembi amesema kuwa zoezi la uunganishaji wa mita hizo linaendelea nchi nzima na zitamwezesha m...

KATA ZA MZINGA, MALANGALI KUPIGA KURA KUCHAGUA MADIWANI KESHO

Image
Na Mwandishi wetu, Dodoma Jumla ya Wapiga Kura 38,151 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura watashiriki katika uchaguzi wa marudio katika Kata za Malangali iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Mkoa wa Rukwa na Mzinga iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.   Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele amesema hayo leo Januari 21, 2026 jijini Ddodoma wakati akisoma risala maalum kuhusu uchaguzi katika Kata hizo utakao fanyika Januari 22, 2026 na kusema kuwa jumla ya vituo 92 vya Kupigia Kura vitatumika.   Aidha, amesema jumla ya wagombea sita (6) kutoka katika vyama vya siasa vitatu (3) wanawania nafasi wazi za udiwani katika maeneo hayo na kuvipongeza vyama vya siasa na wagombea waliojitokeza kushiriki katika uchaguzi huo.   “Kati ya wagombea sita (06), wagombea watano (05) sawa na asilimia 83.3 ni wanaume na mgombea mmoja (01) sawa na asilimia 16.7 ni Mwanamke. Kwa namna ya pekee, Tume inavip...

MRADI WA UMEME JUA KISHAPU UKO MBIONI KUKAMILIKA- MHE SALOME MAKAMBA

Image
  📌Asema jumla ya Megawati 50 kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa  📌Ampongeza Mhe. Rais kwa uwekezaji Mkubwa wa Miradi ya umeme Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amesema Mradi wa Umeme unaozalishwa kwa nguvu ya Jua uliopo Kishapu, Mkoani Shinyanga, uko mbioni kukamilika ambapo jumla ya megawati 50 zinatarajiwa kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa ili kuimarisha upatikanaji wa umeme katika Mkoa wa Shinyanga na mikoa jirani. Mhe. Salome ameyasema hayo Januari 9, 2025, wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya umeme mkoani Shinyanga, ukiwemo Mradi wa Umeme wa Jua Kishapu, Mradi wa upanuzi wa Kituo cha Kupoza Umeme cha Ibadakuli pamoja na Mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Ibadakuli kwenda Mkoa wa Simiyu. Amesema kuwa hadi sasa mradi wa Umeme wa Jua Kishapu umefikia zaidi ya asilimia 89 ya utekelezaji wake na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu, ikiwa ni  jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali  za kuhakikisha nchi inakuwa na umeme wa kuto...

Tutuba: Benki Kuu Yabakiza Riba Asilimia 5.75, Uchumi Waendelea Kuwa Imara.

Image
  Na.Mwandishi wetu. Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel  Tutuba, amesema kuwa Riba ya Benki Kuu (CBR) imebakizwa kuwa asilimia 5.75 kwa robo ya kwanza ya mwaka 2026, huku akieleza kuwa uamuzi huo unalenga kuendeleza utulivu wa uchumi na kuchagiza ukuaji endelevu wa shughuli za kiuchumi nchini. Akizungumza leo Januari 8,2026 Jijini Dar es salaam kufuatia kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha (MPC) kilichofanyika tarehe 7 Januari 2026, Tutuba amesema uamuzi wa kubakiza riba umetokana na mwenendo mzuri wa mfumuko wa bei unaotarajiwa kuendelea kubaki ndani ya lengo la asilimia 3 hadi 5. "Hatua hiyo itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ukuaji wa uchumi, ikiwemo kuimarisha upatikanaji wa mikopo kwa sekta binafsi na kuendeleza uthabiti wa mfumo wa fedha nchini",Amesema. Aidha Gavana ameongeza kuwa Benki Kuu itaendelea kutekeleza sera ya fedha kwa kuhakikisha riba ya mikopo ya siku saba baina ya benki (7-day interbank rate) inabaki ndani ya wigo wa asilimia 3.75 hadi 7.75...

DCEA YATOA RAI KWA WANANCHI KUWA MAKINI NA MIZIGO WANAYOSAFIRISHA BILA KUJUA KILICHOBEBWA.

Image
  Na.Sophia Kingimali. Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na biashara haramu ya dawa za kulevya nchini (DCEA) imetoa wito kwa wananchi kutojihusisha na kusafirisha vifurushi au mizigo wasiyoifahamu, pamoja na kutoa taarifa mapema wanapohisi viashiria vya uvunjifu wa sheria, huku ikisisitiza kuwa itaendelea na operesheni kali nchi nzima dhidi ya wahusika wa biashara hiyo haramu. Akizungumza kuhusu mafanikio ya operesheni zilizofanyika mwezi Desemba 2025,leo Januari 8,2026, Kamishina Jenerali Aretas Lyimo amesema kuwa jumla ya kiasi kikubwa cha dawa za kulevya chenye uzito wa zaidi ya kilogramu 9,683.89 kilikamatwa katika mikoa mbalimbali, huku watuhumiwa kadhaa wakikamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Amesema katika tukio la jijini Dar es Salaam, raia wa Kenya, Kilonzo Mwende (35), alikamatwa katika mtaa wa Bustani, Sinza, akiwa na gramu 131 za heroin. Uchunguzi umebaini kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akiishi nchini tangu mwaka 2023 akijifanya mfanyabiashara wa kuuza chai ya ...